Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 19:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Yesu akamwambia, Ukitaka kuwa mkamilifu, enenda ukauze mali zako, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni; kiisha njoo unifuate.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Yesu akamwambia, “Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze mali yako, uwape maskini fedha hiyo, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Yesu akamwambia, “Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze mali yako, uwape maskini fedha hiyo, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Yesu akamwambia, “Kama unapenda kuwa mkamilifu, nenda ukauze mali yako, uwape maskini fedha hiyo, nawe utakuwa na hazina mbinguni, kisha njoo unifuate.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Isa akamwambia, “Ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Isa akamwambia, “Kama ukitaka kuwa mkamilifu, nenda, ukauze vitu vyote ulivyo navyo, na hizo fedha uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kisha njoo, unifuate.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 19:21
31 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Yule kijima akamwambia, Haya yote nimeyashika tangu utoto wangu: nimepmigukiwa nini tena?


Yule kijana alipolisikia neno lile, akaenda zake kwa huzuni; kwa sababu alikuwa na mali mengi.


Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Akawaambia, Nifuateni, nami nitawafanya kuwa wavuvi wii watu.


Bassi mwe ninyi wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.


Lakini Yesu akamwambia, Nifuate; waache wafu wazike wafu wao.


Yesu alipokuwa anaondoka kutoka huko akaona mtu amekeli fordhani, aitwae Mattayo, akamwambia, Nifuate. Akaondoka, akamfuata.


Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate.


Hatta alipokuwa akipita akamwona Lawi wa Alfayo, ameketi forodhani, akamwambia, Nifuate. Akaondoka akamfuata.


Akawaita makutano na wanafunzi wake, akawaambia, Atakae kuniandama na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Viuzeni mlivyo navyo, katoeni sadaka, jifanyieni mifuko isiyochakaa, akiba isiyopungua katika mbingu, asikokaribia mwizi, wala nondo kuharibu.


Bassi, kadhalika killa mmoja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu.


Na mimi nawaambia ninyi, Jifanyieni rafiki kwa mamona ya udhalimu, illi itakapopunguka wawakaribishe ninyi katika makao ya milele.


Yesu aliposikia haya, akamwambia, Neno moja hujalipata bado; viuze vitu vyote ulivyo navyo, ukawagawie maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni. Kiisha, njoo unifuate.


Baada ya haya akatoka, akaona mtoza ushuru, jina lake Lawi, amekaa forodhani, akamwambia, Nifuate.


Mwanafunzi hampiti mwalimu wake; illa killa aliyekhitimu atakuwa sawa na mwalimu wake.


Akawaamhia wote, Atakae kuniandama, na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake killa siku, anifuate.


Kondoo zangu waisikia sauti yangu, nami nawajua, nao wanifuata;


Mtu akinitumikia, anifuate: nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo; tena mtu akinitumikia, Baba atamheshimu.


wakiuza mali zao, na vitu vyao walivyokuwa navyo, na kuwagawia watu wote kama killa mtu alivyokuwa na haja.


Maana mliwaonea huruma wale waliokuwa katika mafungo, mkakubali kwa furaba kunyangʼauywa mali zenu, mkijua nafsini mwenu kwamba mna mali mbinguni iliyo njema zaidi, idumnyo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo