Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 19:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Mtu mmoja akamwendea akamwambia, Mwalimu mwema, nitende jambo gani jema, illi nipate uzima wa milele?

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mtu mmoja alimjia Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye kitu gani chema ili niupate uhai wa milele?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mtu mmoja alimjia Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye kitu gani chema ili niupate uhai wa milele?”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mtu mmoja alimjia Yesu, akamwuliza, “Mwalimu, nifanye kitu gani chema ili niupate uhai wa milele?”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Mtu mmoja akamjia Isa na kumuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Mtu mmoja akamjia Isa na kumuuliza, “Mwalimu mwema, nifanye jambo gani jema ili nipate uzima wa milele?”

Tazama sura Nakili




Mathayo 19:16
32 Marejeleo ya Msalaba  

Akaweka mikono yake juu yao, akatoka huko.


Yesu akawatazama, akawaambia, Kwa wana Adamu hili haliwezekani; bali kwa Mungu yote yawezekana.


Na killa mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au baba, au mama, au watoto, au mashamba, kwa ajili ya jina langu, atapokea marra mia, na kurithi uzima wa milele.


Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.


nami nawapa uzima wa milele; wala hawatapotea kamwe, wala hakuna mtu atakaewapokonya katika mkono wangu.


Aipendae roho yake ataiangamiza; nae aichukiae roho yake katika ulimwengu huu ataihifadhi hatta uzima wa milele.


illi asipotee mtu aliye yole amwaminiye, bali awe na uzima wa milele.


walakini ye yote atakaekunywa maji yale nitakayompa mimi, hataona kiu milele, bali yale maji nitakayompa yatakuwa ndani yake chemchemi ya maji, yakibubujika hatta uzima wa milele.


Mwayachunguza maandiko, kwa sababu mnadhani kwamba ninyi mna uzima wa milele ndani yake: na hayo ndiyo yanayonishuhudia:


Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi ana uzima wa milele.


Bassi Simon Petro akamjibu, Bwana! twende kwa nani? Wewe una maneno ya uzima wa milele.


kiisha akawaleta nje akasema, Bwana zangu, nifanye nini nipate kuokoka?


wale ambao kwa kustahimili katika kutenda mema wanatafuta utukufu na heshima na kutoa kuharibika, nzima wa milele;


illi, kama vile dhambi ilivyotawaia katika mauti, vivyo hivyo kwa njia ya haki neema itawale hatta uzima wa milele kwa Yesu Kristo Bwana wetu.


Lakini kwa sababu hii nalirehemiwa, illi katika mimi, wa kwanza, Yesu Kristo adhihirishe uvumilivu wote, niwe mfano kwa wale watakaomwamini baadae, wapate uzima wa milele.


Fanya vita vile vizuri vya imani, shika uzima wa milele ulioitiwa, ukayaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.


wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao illi wapate uzima wa milele.


katika tumaini la nzima wa milele, ambao Mungu asiyeweza kusema nwongo aliuahidi kabla ya nyakati za zamani;


tukifanyiziwa wema kwa neema yake, tupate kufanywa warithi wa uzima wa milele, kama lilivyo tumaini letu.


(na uzima buo ulidhihirika, nasi tumeona, na twashuhudu, na twawakhubirini ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);


Na hii ndiyo ahadi alivyowaahidia ninyi, uzima wa milele.


Twajua kwamba Mwana wa Mungu amekwisha kuja, nae ametupa akili illi tumjue yeye aliye wa kweli, nasi tumo ndani yake yeye aliye wa kweli, ndani ya Mwana wake Yesu Kristo. Huyu ndiye aliye Mungu wa kweli na uzima wa milele.


jilindeni katika upendo wa Mungu, mkingojea rehema ya Bwana wetu Yesu Krislo, hatta mpate uzima wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo