Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 18:8 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

8 Mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate, ukautupe mbali nawe; ni vyema zaidi kuingia katika uzima umepungukiwa mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

8 “Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali nawe. Afadhali kwako kuingia katika uhai bila mkono au mguu, kuliko kutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yako miwili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

8 “Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali nawe. Afadhali kwako kuingia katika uhai bila mkono au mguu, kuliko kutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yako miwili.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

8 “Kama mkono au mguu wako ukikukosesha, ukate na kuutupa mbali nawe. Afadhali kwako kuingia katika uhai bila mkono au mguu, kuliko kutupwa katika moto wa milele ukiwa na mikono miwili na miguu yako miwili.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

8 Ikiwa mkono wako au mguu wako unakusababisha utende dhambi, ukate na uutupe mbali. Ni afadhali kwako kuingia katika uzima ukiwa huna mkono mmoja au mguu mmoja, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

Mathayo 18:8
22 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini tusije tukawachukiza, enenda baharini ukatumbukize ndoana, ukatwae samaki yule azukae kwanza; na ukifunua mdomo wake utaona shekeli; ichukue hiyo ukawape kwa ajili yangu na kwa ajili yako.

Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:

Na hawo watakwenda zao kuingia katika adhabu ya milele: bali wenye haki katika uzima wa milele.

Bassi, kadhalika killa mmoja wenu asiyeviacha vitu vyote alivyo navyo hawezi kuwa mwanafunzi wangu.

Akalia, akasema, Baba Ibrahimu, unirehemu, umtume Lazaro, achovye ncha ya kidole chake majini, auburudishe ulimi wangu; kwa maana naumia katika moto huu.

Usiku unakwisha, mchana umekaribia; bassi tuyavue matendo ya giza, tuzivae silaha za nuru.

yeye nae atakunywa mvinyo ya hasira ya Mungu iliyotengenezwa pasipo kuchanganywa na maji katika kikombe cha ghadhabu yake, nae ataumwa kwa moto na kiberiti mbele ya malaika walakalifu na mbele za Mwana kondoo.

Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.

Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, nae waabuduo sanamu, na wawongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndio mauti ya pili.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo