Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 17:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akinena, Msimwambie mtu khabari ya mambo hayo, hatta Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: “Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: “Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Basi, walipokuwa wanashuka mlimani, Yesu akawaonya: “Msimwambie mtu mambo mliyoyaona mpaka Mwana wa Mtu atakapofufuliwa kutoka wafu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Isa akawaagiza, “Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, hadi Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Walipokuwa wakishuka kutoka mlimani, Isa akawaagiza, “Msimwambie mtu yeyote mambo mliyoyaona hapa, mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 17:9
16 Marejeleo ya Msalaba  

akawaagiza wasimdhihirishe;


lakini nawaambieni, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu nae atateswa nao.


Yesu akawaambia, Kwa sababu ya kutokuamini kwenu. Kwa maana, amin, nawaambieni, Mkiwa na imani kama punje ya kharadali mtauambia mlima huu, Ondoka hapa hatta kule; nao utaondoka; wala halitakuwako neno lisilowezekana kwenu.


Walipokuwa wakikaa Galilaya, Yesu akawaambia, Mwana wa Adamu karibu atatiwa mikononi mwa watu,


nao watamwua, na siku ya tatu atafufuka. Wakasikitika sana.


Wakainua macho yao, wasione mtu illa Yesu peke yake.


Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.


Yesu akamwambia, Angalia, usimwambie mtu; illa enenda zako, ukajionyeshe kwa kuhani, utoe sadaka kama alivyoamuru Musa, iwe ushuhuda kwao.


Akawaagiza wasimwambie mtu khabari zake.


Wazazi wake wakastaajabu sana, akawaamuru wasimwambie mtu lililotukia.


Na sauti hii ilipokuja Yesu akaonekana peke yake. Nao wakanyamaza wasimwambie mtu siku zile neno lo lote la hayo waliyoyaona.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo