Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 17:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 akageuka sura yake mbele yao: uso wake ukangʼaa kama jua, mavazi yake yakawa meupe kama nuru.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukangaa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukangaa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Huko, Yesu akageuka sura mbele yao, uso wake ukang'aa kama jua na mavazi yake yakawa meupe kama mwanga.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Wakiwa huko, Isa alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama nuru.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Wakiwa huko, Isa alibadilika sura mbele yao. Uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa na weupe wa kuumiza macho.

Tazama sura Nakili




Mathayo 17:2
17 Marejeleo ya Msalaba  

NA baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, na Yakobo, na Yohana ndugu yake, akawaleta juu ya mlima mrefu peke yao;


Wakawatokea Musa na Eliya, wakizumgumza nae.


Na sura yake ilikuwa kama umeme, na mavazi yake meupe kama thuluji.


akageuka sura yake mbele yao: mavazi yake yakawa yakimetameta, meupe kwa mfano wa thuluji, jinsi asivyoweza fundi duniani kuyafanya meupe.


Ikawa alipokuwa akisali, sura ya uso wake ikageuka, na mavazi yake yakawa meupe, yakimetameta.


Nae Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu, tukautazama utukufu wake, utukufu kama wa Mwana pekee akitoka kwa Baba, amejaa neema na kweli.


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


NIKAONA malaika mwingine hodari akishuka kutoka mbinguni, amevikwa wingu; na upinde wa mvua juu ya kichwa chake: na uso wake kama jua, na miguu yake kama nguzo za moto.


Nikaona kiti eba enzi, cheupe, kikubwa, nae aketiye juu yake; inchi na mbingu zikakimbia nso wake, na mahali pao hapakuonekana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo