Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 16:3 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

3 Na assubuhi, Leo dhoruba; kwa maana uwingu ni mwekundu, na kumetanda. Enyi wanafiki, mnajua kuutamhua uso wa uwingu; hali ishara za zamani hizi hamziwezi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

3 Na alfajiri mwasema: ‘Leo hali ya hewa itakuwa ya dhoruba, maana anga ni jekundu na tena mawingu yametanda!’ Basi, nyinyi mnajua sana kusoma majira kwa kuangalia hali ya anga, lakini kutambua dalili za nyakati hizi hamjui.]

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

3 Na alfajiri mwasema: ‘Leo hali ya hewa itakuwa ya dhoruba, maana anga ni jekundu na tena mawingu yametanda!’ Basi, nyinyi mnajua sana kusoma majira kwa kuangalia hali ya anga, lakini kutambua dalili za nyakati hizi hamjui.]

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

3 Na alfajiri mwasema: ‘Leo hali ya hewa itakuwa ya dhoruba, maana anga ni jekundu na tena mawingu yametanda!’ Basi, nyinyi mnajua sana kusoma majira kwa kuangalia hali ya anga, lakini kutambua dalili za nyakati hizi hamjui.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

3 Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua ishara za nyakati.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

3 Nanyi wakati wa asubuhi mnasema, ‘Leo kutakuwa na dhoruba, kwa sababu anga ni nyekundu na mawingu yametanda.’ Mnajua jinsi ya kupambanua kule kuonekana kwa anga, lakini hamwezi kupambanua dalili za nyakati.

Tazama sura Nakili




Mathayo 16:3
11 Marejeleo ya Msalaba  

vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakasika, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa, na maskini wanakhubiriwa khabari njema.


Enyi wanafiki, ni vyema alivyotabiri Isaya katika khabari zenu, akinena,


Lakini Yesu akaufahamu uovu wao, akasema, Mbona mnanijaribu, enyi wanafiki?


Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.


Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu.


Mnaflki, iondoe kwanza ile boriti katika jicho lako; ndipo utakapoona sana hatta kukiondoa kibanzi katika jicho la ndugu yako.


Ole wenu, maana mfano wenu ni makaburi yasiyoonekana, na watu wapitao juu yao hawana khabari.


Enyi wanafiki, mwajua kuufasiri uso wa inchi na mbingu; imekuwaje, bassi, hamjui kuyafasiri majira haya?


Bassi Bwana akamjibu, akasema, Ewe mnafiki, killa mmoja wenu je! hamfungui ngʼombe wake au punda wake mazizini siku ya sabato, akaenda nae kumnywesha?


Lakini chakula kigumu in cha watu wazima, ambao akili zao, kwa kutumiwa, zimezoezwa kupambanua mema na mabaya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo