Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 16:26 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

26 Kwa maana atafaidiwa mtu nini akiupata ulimwengu wote, na kupata khasara ya roho yake? au mtu atatoa nini badala ya roho yake?

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

26 lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

26 lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

26 lakini mtu anayeyapoteza maisha yake kwa ajili yangu, atayapata. Je, mtu atafaidi nini akiupata utajiri wote wa ulimwengu na hali amepoteza maisha yake? Au, mtu atatoa kitu gani kiwe badala ya maisha yake?

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

26 Kwa maana itamfaidi mtu nini kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

26 Kwa maana, je, itamfaidi nini mtu kuupata ulimwengu wote, lakini akayapoteza maisha yake? Au mtu atatoa nini badala ya nafsi yake?

Tazama sura Nakili

Mathayo 16:26
11 Marejeleo ya Msalaba  

Maana mtu atakae kuisalimisha roho yake, ataiangamiza; na mtu atakaeitoa roho yake kwa ajili yangu, ataiona.

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.

Jicho lako la kuume likikukosesha, lingʼoe ulitupe mbali nawe: kwa maana yakufaa kiungo chako kimoja kipotee wala mwili wako mzima usitupwe katika jehannum.

Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo, wanakutaka roho yako. Nayo uliyojiwekea tayari yatakuwa ya nani?

Ibrahimu akasema, Mwanangu, kumbuka ya kuwa ulipokea mema yako katika maisha yako, na Lazaro kadhalika mabaya; lakini sasa yeye yupo hapa anafarajiwa, nawe unanmizwa.

Maana itamfaidia mtu nini kuupata ulimwengu wote na kujipoteza, au kupata khasara ya roho yake?

Tufuate:

Matangazo

Matangazo