Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 16:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Wakati huo Yesu aliwaambia wanafunzi wake, Mtu atakae kuandama nyuma yangu, ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Kisha Yesu akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kuwa mfuasi wangu, lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Ndipo Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Ndipo Isa akawaambia wanafunzi wake, “Mtu yeyote akitaka kunifuata, ni lazima ajikane mwenyewe, auchukue msalaba wake, anifuate.

Tazama sura Nakili




Mathayo 16:24
18 Marejeleo ya Msalaba  

Nae asiyechukua msalaba wake na kufuata nyuma yangu, hanifai.


Hatta walipokuwa wakitoka humo, wakakutana na mtu Mkurene, jina lake Simon; huyu wakamtumikisha auchukue msalaba wake.


Yesu akamkazia macho, akampenda, akamwambia, Umepungukiwa neno moja Enenda, ukauze ulivyo navyo vyote, uwape maskini, nawe utakuwa na hazina mbinguni: ukiisha, njoo ukajitwike msalaba wako unifuate.


Wakamtumikisha mtu aliyekuwa akipita, Simon Mkurene, akitoka mashamba, baba wa Iskander na Rufo, auchukue msalaba wake.


Akawaita makutano na wanafunzi wake, akawaambia, Atakae kuniandama na ajikane nafsi yake, ajitwike msalaba wake, anifuate.


Na mfu ye yote asiyechukua msalaba wake na kuja nyuma yangu, hawezi kuwa mwanafunzi wangu.


Walipokuwa wakimchukua, wakamshika Mkurene Simon, aliyekuwa akitoka shamba, wakamtwika yeye msalaba, auchukue nyuma yake Yesu.


akatoka, akijichukulia msalaba wake, hatta mahali paitwapo pa kichwa, na kwa Kiebrania Golgotha;


Akasema hili kwa kuonyesha ni mauti gani atakayomtukuza Mungu. Na akiisha kusema haya, akamwambia, Nifuate.


Yesu akamwambia, Nikitaka huyu akae hatta nijapo imekukhusu nini? wewe unifuate mimi.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Sasa nayafurahia mateso niliyo nayo kwa ajili yenu; tena natimiliza yale yaliyopungua ya mateso ya Kristo katika mwili wangu, kwa ajili ya mwili wake, yaani, kanisa lake,


mtu asifadhaishwe na mateso haya: maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa haya.


Naam, na wote wapendao kuishi maisha ya ntawa katika Kristo Yesu wataudhiwa.


Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo nae aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo