Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 16:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Toka wakati huo Yesu akaanza kuwaonya wanafunzi wake ya kwamba imempasa kwenda Yerusalemi, na kuteswa mengi na wazee na makuhani wakuu, na waandishi, na kuuawa, na siku ya tatu kufufuka.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwazi wanafunzi wake kwamba ni lazima aende Yerusalemu, na huko kupata mateso mengi yatakayosababishwa na wazee, makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Kwamba, atauawa na siku ya tatu atafufuliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwazi wanafunzi wake kwamba ni lazima aende Yerusalemu, na huko kupata mateso mengi yatakayosababishwa na wazee, makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Kwamba, atauawa na siku ya tatu atafufuliwa.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwajulisha waziwazi wanafunzi wake kwamba ni lazima aende Yerusalemu, na huko kupata mateso mengi yatakayosababishwa na wazee, makuhani wakuu na waalimu wa sheria. Kwamba, atauawa na siku ya tatu atafufuliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 Tangu wakati huo, Isa alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa Torati, na kwamba itampasa auawe, lakini siku ya tatu kufufuliwa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 Tangu wakati huo, Isa alianza kuwaeleza wanafunzi wake kwamba hana budi kwenda Yerusalemu na kupata mateso mengi mikononi mwa wazee, viongozi wa makuhani, na walimu wa Torati, na kwamba itampasa auawe lakini siku ya tatu kufufuliwa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 16:21
31 Marejeleo ya Msalaba  

Maana kama vile Yunus alivyokuwa siku tatu mchana na nsiku katika tumbo la nyamgumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa inchi.


Petro akamchukua, akaanza kumkemea, akinena, Hasha, Bwana, haya hayatakupata.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


lakini nawaambieni, ya kwamba Eliya amekwisha kuja, wasimtambue, wakamtenda yote waliyotaka. Vivyo hivyo Mwana wa Adamu nae atateswa nao.


Na walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaagiza, akinena, Msimwambie mtu khabari ya mambo hayo, hatta Mwana wa Adamu atakapofufuka katika wafu.


kama vile Mwana wa Adamu asivyokuja kukhudumiwa, bali kukhudumu, na kutoa roho yake kuwa dia ya wengi.


Mwajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa apate kusulibiwa.


Hatta alipokuwa akisema, Yuda, mmoja wa wale thenashara akaja, na pamoja nae makutano mengi, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu na wazee wa watu.


Aliposhitakiwa na makuhani wakuu na wazee, hakujibu hatta neno.


wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka.


Hayupo hapa; kwa maana amefufuka kama alivyosema. Njoni, patazameni mahali alipolazwa Bwana.


Akaanza kuwafundisha kwamba imempasa Mwana wa Adamu kupata mateso mengi, na kukataliwa na wazee, na makuhani, wakuu na waandishi, na kuuawa, na baada ya siku tatu kufufuka.


Akajihu akawaambia, Ni kweli Eliya yuaja kwanza, na kutengeneza yote; lakini, pamoja na haya ameandikwaje Mwana wa Adamu ya kwamba atateswa mengi na kudharanliwa?


Lakini kwanza hana buddi kupata mateso mengi, na kukataliwa na kizazi biki.


Akawaambia, Ndivyo ilivyoandikwa, na ndivyo ilivyompasa Kristo kuteswa, na kufufuka siku ya tatu;


walioonekana katika utukufu, wakanena khahari ya kufariki kwake atakakotimiza Yerusalemi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo