Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 16:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na jun ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Nami nakuambia: Wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala nguvu za kifo hazitaweza kulishinda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Nami nakuambia: Wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala nguvu za kifo hazitaweza kulishinda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Nami nakuambia: wewe ni Petro, na juu ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; wala nguvu za kifo hazitaweza kulishinda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu nitajenga jumuiya ya wafuasi wangu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kuwashinda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Nami nakuambia, wewe ndiwe Petro, na juu ya mwamba huu nitajenga jumuiya ya wafuasi wangu, hata malango ya Kuzimu hayataweza kuwashinda.

Tazama sura Nakili




Mathayo 16:18
42 Marejeleo ya Msalaba  

Na majina ya mitume thenashara ni haya: Wa kwanza Simon aliyekwitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake;


Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo.


Na asipowasikiliza wao, liambie kanisa: na asipolisikiliza kanisa pia, na awe sawasawa na mtu wa Mataifa na mtoza ushuru.


Nae Yesu akitembea kando ya bahari ya Galilaya, akaona ndugu wawili, Simon aitwae Petro, na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; maana walikuwa wavuvi.


Bassi killa asikiae haya maneno yangu, na kuyafanya, nitamfananisha na mtu mwenye akili aliyejenga nyumba vake juu ya mwamba:


Akampeleka kwa Yesu. Yesu akamtazama, akasema, Wewe Simon, mwana wa Yona, utakwitwa Kefa (tafsiri yake, Petro).


wakimsifu Mungu, na kuwapendeza wutu wote. Bwana akalizidisha kanisa killa siku kwa wale waliokuwa wakiokolewa.


Jiangalieni nafsi zenu, na kundi lote, ambalo Roho Mtakatifu aliwakabidhi mlisimamie, kanisa lake Mungu, alilojipatia kwa damu yake mwenyewe.


NA Saul alikuwa akiona vema auawe. Siku ile kukatukia adha nyingi juu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wote wakatawanyika katika inchi ya Yahudi na Samaria, illa mitume.


U wapi, mauti, uchungu wako? Ku wapi, kaburi, kushinda kwako?


tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


illi sasa, kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka ya mbinguni;


Hii ni siri kubwa; lakini nanena khabari ya Kristo na Kanisa.


Nae ni kichwa cha mwili, yaani cha kanisa; nae ni mwanzo, ni mzaliwa wa kwanza katika wafu, illi awe mtangulizi katika yote.


Lakini nikikawia, upate kujua sana jinsi iwapasavyo watu kuenenda katika nyumba ya Mungu iliyo kanisa la Mungu aliye hayi, nguzo na msingi wa kweli.


(mtu asiyejua kuisimamia nyumba yake mwenyewe, atalitunzaje kanisa la Mungu?)


Bassi tukipokea ufalme usioweza kutetemeshwa, tuwe na neema, illi kwa hiyo tumtolee Mungu ibada ya kumpendeza, pamoja na unyenyekevu na kicho:


Malaika wa saha akapiga baragumu, pakawa sauti kuu katika mbingu, zikisema, Falme za dunia zimekwisha kuwa ufalme na Mungu na wa Kristo wake, nae atamiliki hatta milele na milele.


Na ukuta wa mji una misingi thenashara, na katika ile misingi majina theriashara ya mitume wa Mwana kondoo.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo