Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 15:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Yesu akawaita wanafunzi wake, akasema, Nawahurumia makutano, kwa kuwa yapata siku tatu wamekaa pamoja nami, hawana kitu cha kula: na kuwaaga wakifunga sitaki, wasije wakazimia njiani.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema, “Nawaonea huruma watu hawa kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu, wala hawana chakula. Sipendi kuwaacha waende zao bila kula, wasije wakazimia njiani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema, “Nawaonea huruma watu hawa kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu, wala hawana chakula. Sipendi kuwaacha waende zao bila kula, wasije wakazimia njiani.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Basi, Yesu aliwaita wanafunzi wake, akasema, “Nawaonea huruma watu hawa kwa sababu wamekuwa nami kwa siku tatu, wala hawana chakula. Sipendi kuwaacha waende zao bila kula, wasije wakazimia njiani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Kisha Isa akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Ninahurumia umati huu wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa pamoja nami kwa muda wa siku tatu, na hawana chakula chochote. Nami sipendi kuwaaga watu wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Kisha Isa akawaita wanafunzi wake, akawaambia, “Ninauhurumia huu umati wa watu, kwa sababu sasa wamekuwa pamoja nami kwa muda wa siku tatu, na hawana chakula chochote. Nami sipendi kuwaaga wakiwa na njaa, wasije wakazimia njiani.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 15:32
17 Marejeleo ya Msalaba  

Maana kama vile Yunus alivyokuwa siku tatu mchana na nsiku katika tumbo la nyamgumi, hivyo ndivyo Mwana wa Adamu atakavyokuwa siku tatu mchana na usiku katika moyo wa inchi.


Yesu aliposikia, akatoka huku katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, kwa faragha. Na makutano waliposikia, wakamfuata kwa miguu toka miji yao.


Wanafunzi wake wakamwambia, Tupate wapi mikate mingi hapa nyikani, hatta kushibisha makutano mengi namna hii?


Yesu akawahurumia, akawagusa macho yao; marra macho yao yakapata kuona, wakamfuata.


wakinena, Bwana, tumekumbuka kwamba yule mjanja alisema, alipokuwa hayi bado, Baada ya siku tatu nitafufuka.


Na alipowaona makutano, akawahurumia, kwa maana walikuwa wamechoka na kutawanyika kama kondoo wasio na mchunga.


Na marra nyingi amemtupa katika moto, na katika maji, amwangamize; lakini ukiweza neno, utuhurumie, utusaidie.


Na Bwana alipomwona, akamhurumia, akamwambia, Usilie.


Na kulipokuwa kukipambazuka Paolo akawasihi wote wale chakula, akisema, Leo ni siku ya kumi na nne kungoja na kufunga, hamkula kitu cho chote.


Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo