Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 15:31 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

31 hatta makutano wakastaajabu, walipowaona bubu wanasema, vilema wanakuwa wazima, viwete wanakwenda, na vipofu wanaona; wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

31 Umati ule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubu wakiongea, waliokuwa wamelemaa wamepona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; watu wakamsifu Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

31 Umati ule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubu wakiongea, waliokuwa wamelemaa wamepona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; watu wakamsifu Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

31 Umati ule wa watu ulishangaa sana ulipoona bubu wakiongea, waliokuwa wamelemaa wamepona, viwete wakitembea na vipofu wakiona; watu wakamsifu Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

31 Hao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

31 Hao watu wakashangaa walipoona bubu wakisema, vilema wakipona, viwete wakitembea na vipofu wakiona, wakamtukuza Mungu wa Israeli.

Tazama sura Nakili




Mathayo 15:31
23 Marejeleo ya Msalaba  

Wakamwendea makutano mengi walio na viwete, vipofu, bubu, vilema, na wengine wengi pamoja nao, wakawaweka miguuni pa Yesu; akawaponya;


Mkono wako au mguu wako ukikukosesha, ukate, ukautupe mbali nawe; ni vyema zaidi kuingia katika uzima umepungukiwa mkono au mguu, kuliko kuwa na mikono miwili au miguu miwili, na kutupwa katika moto wa milele.


Vipofu na viwete wakamwendea hekaluni, akawaponya.


Yesu aliposikia haya, akastaajabu, akawaambia wale waliomfuata, Amin, nawaambieni, Sijaona imani kubwa kama hii, hatta katika Israeli.


Hatta wale walipokuwa wakitoka, wakamletea mtu bubu mwenye pepo.


Na pepo alipofukuzwa, yule bubu akasema, makutano wakastaajabu, wakanena, Haijaonekana hivi katika Israeli wakati wo wote.


Makutano wakimwona, wakastaajabu, wakamtukuza Mungu, aliyewapa watu mamlaka ya jinsi hii.


Akaondoka marra, akajitwika kitanda chake, akatoka mbele yao wote; hatta wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakinena, Namna hii hatujapata kuyaona kamwe.


Ametenda yote vizuri; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.


Na mkono wako ukikukosesha, ukate; ni kheri kuiingia katika uzima u kilema, kuliko kuwa na mikono miwili, na kwenda zako jehannum, kwenye moto usiozimika;


Bali ufanyapo karamu, wakaribishe maskini, vilema, viwete, vipofu: nawe utakuwa kheri:


Yule mtumishi akaenda, akamwarifu Bwana wake mambo haya. Ndipo yule mwenye nyumba akaghadhabika, akamwambia mtumishi wake, Toka upesi ukaende njia kuu na vichochoro vya mji, ukalete hapa maskini, na vilema, na viwete, na vipofu.


Marra akapata kuona, akamfuata, akimtukuza Mungu; na watu wote walipoona wakampa Mungu sifa.


Khofu ikawashika wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Nabii mkuu ametokea kwetu: na Mungu amewajilia watu wake.


Bassi marra ya pili wakamwita yule mtu aliyekuwa kipofu wakamwambia, Mpe Mungu utukufu. Sisi tunajua ya kuwa mtu huyu ni mwenye dhambi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo