Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 14:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Akawaagiza makutano waketi katika majani; akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akabariki, akamega, akawapa wanafunzi ile mikate, wanafunzi wakawapa makutano.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Akawaamuru watu waketi katika nyasi. Kisha Yesu akaitwaa ile mikate mitano na wale samaki wawili, akatazama juu mbinguni, akavibariki. Halafu akaimega hiyo mikate, akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Isa akaagiza umati wa watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia ule umati.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Isa akaagiza makutano wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akavibariki na kuimega ile mikate. Kisha akawapa wanafunzi, nao wanafunzi wakawagawia makutano.

Tazama sura Nakili




Mathayo 14:19
24 Marejeleo ya Msalaba  

Akasema, Nileteeni vitu vile hapa.


Akawaagiza wawaketishe wote, vikao vikao, penye majani mabiehi.


Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama mbinguni, akavibariki, akaimega ile mikate, akawapa wanafunzi wake awaandikie: na zile samaki mbili akawagawia wote.


akatazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Effatha, maana yake, Funguka!


Akakipokea kikombe, akashukuru, akasema: Twaeni hiki mkagawanye ninyi kwa ninyi;


Akatwaa mkate, akashukuru, akaumega, akawapa, akisema, Huu ni mwili wangu unaotolewa kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangu.


Ikawa, akiketi pamoja nao, akautwaa mkate, akaubariki, akaumega, akawagawia.


Kwa maana walikuwako wanaume wapata elfu tano.


Wakafanya hivi, wakawaketisha wote. Akaitwaa ile mikate mitano na zile samaki mbili, akatazama juu mbinguni, akavibariki, akavimega, akawapa wanafunzi, kuviweka mbele ya makutano.


Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.


(lakini mashua nyingine zilikuja kutoka Tiberia karibu na pahali pale walipokula mikate, wakati Bwana aiiposhukuru);


Alipokwisha kusema haya akatwaa mkate, akamshukuru Mungu mbele yao wote akaumega akaanza kula.


Yeye aadhimishae siku, kwa Bwana aiadhimisha; na yeye asiyeadhimisha siku, haiadhimishi kwa Bwana; nae alae, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; nae asiokula, hali kwa Bwana, nae amshukuru Mungu.


Kikombe kile cha baraka tukibarikicho, je! si ushirika wa damu ya Kristo? Mkate ule timmegao, si ushirika wa mwili wti Kristo?


Bassi, mlapo, au mnywapo, au mtendapo neno lo lote, fanyeni yote kwa utukufu wa Mungu.


na akiisha kushukuru akaumega, akasema, Huu ndio mwili wangu ulio kwa ajili yenu; fanyeni hivi kwa ukumbusho wangii.


Na killa mfanjalo, kwa neno au kwa tendo, fanyeni yote katika jina la Bwana Yesu, mkimshukuru Mungu Baba kwa yeye.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo