Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 14:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Hatta ilipokuwa jioni, wanafunzi wake wakamwendea, wakanena, Mahali hapa nyika tupu, na saa imekwisha pita; waage makutano, waende zao vijijini, wakajinunulie vyakula.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kulipokuwa jioni, wanafunzi wake walimwendea wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na saa za mchana zimepita. Basi, uwaage watu ili waende vijijini wakajinunulie chakula.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makundi ya watu ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walienda kwake, wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na muda sasa umekwisha. Waage makutano ili waende zao vijijini wakajinunulie chakula.”

Tazama sura Nakili

Mathayo 14:15
7 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu aliposikia, akatoka huku katika chombo, akaenda mahali pasipo watu, kwa faragha. Na makutano waliposikia, wakamfuata kwa miguu toka miji yao.

Yesu akatoka, akaona makutano mengi, akawahurumia, akawaponya wagonjwa wao.

Yesu akawaambia, Hawana haja kwenda zao, wapeni ninyi kula.

Nae hakumjibu neno. Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwomba, wakinena. Mwache aende zake; kwa maana anapiga kelele nyuma yetu.

hatta nikiwaaga waende zao nyumbani kwao wanafunga, watazimia njiani: na baadhi yao wametoka mbali.

Hatta jua lilipoanza kuchwa wale thenashara wakamwendea wakamwambia, Uwaage makutano illi waende zao hatta vijiji vilivyo kandokando na mashamba wakapate mahali pa kulala na vyakula: maana hapa tulipo nyika tupu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo