Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 13:52 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

52 Akawaambia, Kwa sababu hii, killa mwandishi mwenye elimu ya ufalme wa mbinguni amefanana na mtu mwenye nyumba atoae katika hazina yake vitu vipya na vya kale.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

52 Naye akawaambia, “Hivyo basi, kila mwalimu wa sheria anayekuwa mwanafunzi wa ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

52 Naye akawaambia, “Hivyo basi, kila mwalimu wa sheria anayekuwa mwanafunzi wa ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

52 Naye akawaambia, “Hivyo basi, kila mwalimu wa sheria anayekuwa mwanafunzi wa ufalme wa mbinguni anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

52 Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa Torati aliyefundishwa elimu ya ufalme wa mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

52 Akawaambia, “Basi kila mwalimu wa Torati aliyefundishwa elimu ya Ufalme wa Mbinguni ni kama mwenye nyumba anayetoa kutoka ghala yake mali mpya na mali ya zamani.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 13:52
31 Marejeleo ya Msalaba  

Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa mema: na mtu mbaya katika hazina yake mbaya hutoa mabaya,


Yesu aliwaambia, Mmeyafahamu haya yote? Wakamwambia, Naam, Bwana.


Ikawa Yesu alipomaliza mifano hii, akatoka, akaenda zake.


Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji;


Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Na kwa hiyo hekima ya Mungu ilisema, Nitatuma kwao manabii na mitume, na wataua baadhi yao, na kuwaudhi,


Amri mpya nawapeni, mpendane; kama vile nilivyowapenda ninyi, na ninyi mpendane vivyo hivyo.


kama wenye huzuni, bali siku zote wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali wenye vitu vyote.


kwa hayo, myasomapo, mtaweza kutambua ufahamu wangu katika siri yake Kristo;


Mimi, niliye mdogo kuliko yeye aliye mdogo wa watakatifu wote, nilipewa neema hii, kuwakhubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika;


kama mlivyofundishwa na Epafra mjoli wetu mpenzi, aliye mkhudumu amini wa Kristo kwa ajili yenu;


Neno la Kristo likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; kwa neema mkimwimbia Bwana mioyoni mwenu.


si mtu aliyeongoka karibu, asije akajivuna, akaanguka katika hukumu ya Shetani.


alishikae neno la imani kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupingana nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo