Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 13:38 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

38 na lile konde ni ulimwengu; na zile mbegu njema ni wana wa ufalme; na yale magugu ni wana wa yule mwovu;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

38 Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

38 Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

38 Lile shamba ni ulimwengu. Zile mbegu nzuri ni watu wale ambao ufalme ni wao. Lakini yale magugu ni wale watu wa yule Mwovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

38 Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

38 Shamba ni ulimwengu na mbegu nzuri ni wana wa Ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 13:38
27 Marejeleo ya Msalaba  

Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani.


Na injili hii ya ufalme itakhubiriwa katika ulimwengu wote, kuwa ushuhuda kwa mataifa yote; ndipo ule mwisho utakapokuja.


Bali maneno yenu yawe, Ndio, ndio; Sio, sio: kwa kuwa izidiyo haya yatoka kwa yule mwovu.


bali wana wa ufalme watatupwa katika giza la nje; ndiko kutakuwa kilio na kusaga meno.


na mataifa yote wakhubiriwe kwa jina lake toba na ondoleo la dhambi, kuanzia Yerusalemi.


Amin, amin, nawaambieni, Punje ya nganu isipoanguka katika inchi ikafa, hukaa katika hali ya peke yake; bali ikifa, hutoa mazao mengi.


Ninyi wa baba yenu Shetani, na tamaa za baba yenu ndizo mpendazo kuzifanya. Yeye alikuwa mwuaji tangu mwanzo, wala hakusimama katika kweli kwa kuwa kweli hamna ndani yake. Asemapo uwongo, husema yaliyo yake mwenyewe, kwa sababu yu mwongo, na baba ya huo.


Ewe mwenye kujaa hila na uovu wote, mwana wa shetani, adui wa haki yote, huachi kuzipotoa njia za Bwana zilizonyoka?


Lakini nasema, Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imetoka ikaenea katika inchi yote, Na maneno yao hatta miisho ya ulimwengu.


ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulika na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, illi waitii imani;


kama tu watoto, bassi, tu warithi; warithi wa Mungu, warithio pamoja na Kristo; naam, tukiteswa pamoja nae illi tutukuzwe pamoja nae.


iliyofika kwenu, kama ilivyo katika ulimwengu wote, ikizaa matunda na kukua, kama na inavyokua kwenu, tangu siku mliposikia nikaifahamu sana neema ya Mungu katika kweli;


Alipopenda alituzaa sisi kwa neno la kweli, tuwe kama limhuko la viumbe vyake.


Sikihzeni, ndugu niwapendao, Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


Wapenzi, sasa tu wana wti Mungu, wala haijadhihirika bado tutakidokuwa: lakini twajua ya kuwa akidhihiri, tutafanana nae; kwa maana tutamwona kama alivyo.


Nikaona malaika niwingine akiruka kati kati ya mbingu, mwenye injili ya milele, awakhubiri wakaao juu ya inchi na killa taifa na kabila na lugha na jamaa,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo