Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 13:35 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

35 illi litimizwe neno lililonenwa mi nabii, akisema, Nitafunua kinywa changu kwa mifano, Nitatoa mambo yaliyostirika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

35 ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema nao kwa mifano; nitafichua yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

35 ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema nao kwa mifano; nitafichua yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

35 ili jambo lililonenwa na nabii litimie: “Nitasema nao kwa mifano; nitafichua yaliyofichika tangu kuumbwa ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

35 Hii ilikuwa ili kutimiza neno lililonenwa na nabii, aliposema: “Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano; nitahubiri mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

35 Hii ilikuwa ili kutimiza lile lililonenwa kwa kinywa cha nabii aliposema: “Nitafungua kinywa changu niseme nao kwa mifano; nitahubiri mambo yaliyofichika tangu kuumbwa kwa misingi ya ulimwengu.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 13:35
24 Marejeleo ya Msalaba  

Na neno la nabii Isaya linatimia kwao, likinena, Kusikia mtasikia, wala hamtafahamu; Mkitazama mtatazama, wala hamtaona:


Akasema nao mengi kwa mifano, akinena, Mpanzi alitoka kwenda kupanda mbegu.


Kisha Mfalme atawaambia wale walio mkono wake wa kuume, Njoni, mliobarikiwa wa Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tangu kuumbwa ulimwengu:


akafunua kinywa chake, akawafundisha, akinena,


Lakini itakuwa rakhisi Turo na Sidoni istahimili adhabu zao siku ile ya hukumu, kuliko ninyi.


Baba, hao nao ulionipa, nataka wawe pamoja nami nilipo, wapate kuutazama utukufu wangu ulionipa; kwa maana ulinipenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.


Kazi zake zote zimejulika na Mungu tangu mwanzo wa ulimwengu.


bali twanena hekima ya Mungu katika fumbo, ile iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu asili, kwa utukufu wetu;


ambayo hawakujulishwa wana Adamu katika vizazi vingine, jinsi walivyofunuliwa zamani hizi mitume wake watakatifu na manabii katika Roho;


na kuwaangaza watu wote, wajue khabari ya kuishiriki siri ile, ambayo tangu zamani zote ilisetirika katika Mungu, aliyeviumba vyote kwa Yesu Kristo:


KWA sehemu nyingi na kwa namna nyingi Mungu zamani alisema na babu zetu katika manabii,


Watu wote wakaao juu ya inchi wakamsujudu, ambao majina yao hayakuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana kondoo aliyechinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya dunia.


Yule nyama uliyemwona alikuwako, nae hayuko, nae yu tayari kupanda katika abuso na kwenda kwenye uharibifu. Nao wakaao juu ya inchi, wasioandikwa majina yao katika kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, watataajabu wamwonapo yule nyama, ya kwamba alikuwako, nae hayuko, nae atakuwako.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo