Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 13:33 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

33 Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke, akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

33 Yesu akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga madebe mawili na nusu, hata unga wote ukaumuka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

33 Yesu akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga madebe mawili na nusu, hata unga wote ukaumuka.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

33 Yesu akawaambia mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mama mmoja, akaichanganya na unga madebe mawili na nusu, hata unga wote ukaumuka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

33 Akawaambia mfano mwingine, “Ufalme wa mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga hadi wote ukaumuka.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

33 Akawaambia mfano mwingine, “Ufalme wa Mbinguni unafanana na chachu ambayo mwanamke aliichukua akaichanganya katika kiasi kikubwa cha unga mpaka wote ukaumuka.”

Tazama sura Nakili




Mathayo 13:33
19 Marejeleo ya Msalaba  

Akawatolea mfano mwingine, akinena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake:


Na kama Bwana asingalizikatiza siku zile, asingeokoka mtu aliye yote; lakini kwa ajili ya wateule aliowateua amezikatiza siku zile.


Umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia.


Kilia tawi ndani yangu lisilozaa huliondoa; na killa lizaalo hulisafisha illi lizidi kuzaa.


Chachu kidogo huchachua donge nzima.


niliaminilo ndilo hili, ya kwamba yeye aliyeanza kazi njema mioyoni mwenu ataimaliza hatta siku ya Yesu Kristo;


Na hii ndiyo sala yangu, pendo lenu lizidi kuwa jingi sana, katika hekima na ufahamu wote;


Lakini, kaeni katika neema, na katika kumjua Bwana wetu, Mwokozi wetu, Yesu Kristo. Utukufu una yeye sasa na hatta milele. Amin.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo