Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 13:30 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

30 Viacheni vyote vikue hatta wakati wa mavuno: na wakati wa mavuno nitawaambia wavimao, Yakusanyeni kwanza magugu, myafunge matita matita, mkayachome; bali nganu ikusauyeni ghalani mwangu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

30 Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: Kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

30 Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: Kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu.’”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

30 Acheni vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji: kusanyeni kwanza magugu mkayafunge mafungumafungu ya kuchomwa. Lakini ngano ikusanyeni mkaiweke ghalani mwangu.’”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

30 Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja hadi wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

30 Acheni ngano na magugu vikue vyote pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati huo nitawaambia wavunaji wayakusanye magugu kwanza, wayafunge matita matita ili yachomwe moto; kisha wakusanye ngano na kuileta ghalani mwangu.’ ”

Tazama sura Nakili




Mathayo 13:30
20 Marejeleo ya Msalaba  

lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya nganu, akaenda zake.


Akasema, La; labuda wakati wa kukusanya magugu, mtangʼoa na nganu pamoja nayo.


na mataifa yote watakusanyika mbele yake: nae atawabagua kama vile mchunga abaguavyo kondoo na mbuzi:


Kisha atawaambia na wale walio mkono wake wa kushoto, Ondokeni kwangu, mliolaaniwa, kwenda katika moto wa milele, aliowekewa tayari Shetani na malaika zake:


Pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; atakusanya nganu yake ghalani, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.


pepeto lake li mkononi mwake, nae ataitakasa sana sakafu yake; afakusanya nganu yake ghalani mwake, bali makapi atayateketeza kwa moto usiozimika.


Mtu asipokaa ndani yangu, atupwa nje kama tawi, akauka; huyakusanya, huyatupa motoni, yakateketea.


Bassi msihukumu neno kabla ya wakati wake, mpaka ajapo Bwana; nae atayamulika yaliyosetirika ya giza, na kuyadhihirisha mashauri ya mioyo; ndipo killa mtu atakapoipata sifa yake kwa Mungu.


Dhambi za watu wengine ni dhahiri, zatangulia kwenda hukumuni; wengine dhamhi zao zawafuata.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo