Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 13:24 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

24 Akawatolea mfano mwingine, akinena, Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu aliyepanda mbegu njema katika konde lake:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

24 Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

24 Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

24 Yesu akawaambia watu mfano mwingine: “Ufalme wa mbinguni unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

24 Isa akawaambia mfano mwingine, akasema: “Ufalme wa mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

24 Isa akawaambia mfano mwingine, akasema: “Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake.

Tazama sura Nakili




Mathayo 13:24
23 Marejeleo ya Msalaba  

Killa alisikiae neno la ufalme asifahamu, huja yule mwovu, akaliteka lililopandwa moyoni mwake. Huyu ndiye aliyepandwa njiani.


lakini watu walipolala, akaja adui yake akapanda magugu katikati ya nganu, akaenda zake.


Akawatolea mfano mwingine, akisema, Ufalme wa mbinguni umefanana na punje ya kharadali, aliyotwati mtu akaipanda katika shamba lake;


Akawaambia mfano mwingine; Ufalme wa mbinguni umefanana na chachu aliyotwaa mwanamke, akaisetiri katika pishi tatu za unga, hatta ukachacha wote pia.


Akajibu, akasema, Azipandiie zile mbegu njema ni Mwana wa Adamu;


Tena ufalme wa mbinguni umefanana na juya, lililotupwa baharini, likakusanya za killa namna:


Kwa sababu hii ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyetaka kufanya hesabu na watumisbi wake.


KWA maana ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu.


Sikilizeni mfano mwingine. Kulikuwa na mtu mwenye nyumba, nae alipanda mizabibu, akazungusha uzio, akachimba shimo ndani yake, akajenga mnara, akapangisha wakulima, akasafiri.


Ufalme wa mbinguni umefanana na mfalme mmoja aliyemfanyia mwana wake arusi.


NDIPO ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu.


Bassi, akasema, Ufalme wa Mungu umefanana na nini? Na niufananishe na nini?


Akasema marra ya pili, Niufananishe na nini ufalme wa Mungu?


kwa sababu ya tumaini mlilowekewa akiba mbinguni, khabari zake mlisikia zamani kwa neno la kweli ya Injili;


kwa kuwa mmezaliwa marra ya pili, si kwa mbegu iharibikayo, bali isiyoharibika, kwa neno la Mungu lenye uzima, na lidumulo hatta milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo