Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 13:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye hilo neno, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali hulisonga neno hilo, naye hazai matunda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye hilo neno, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali hulisonga neno hilo, naye hazai matunda.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Ile mbegu iliyoanguka kati ya miti ya miiba, ni mfano wa mtu asikiaye hilo neno, lakini wasiwasi wa ulimwengu huu na anasa za mali hulisonga neno hilo, naye hazai matunda.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu anayelisikia neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Ile mbegu iliyopandwa katika miiba ni yule mtu alisikiaye neno, lakini masumbufu ya maisha haya na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno na kulifanya lisizae matunda.

Tazama sura Nakili




Mathayo 13:22
42 Marejeleo ya Msalaba  

Na killa mtu atakaenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakaenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ntakaokuwa.


na yule adui aliyeyapanda ni shetani; na mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.


Bassi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii.


Nyingine zikaanguka penye miiba; miiba ikamea, ikazisonga:


Akawaambia, Angalieni, jilindeni na kutamani, maana uzima wa mtu hautoki katika mali zake, kwa sababu ana wingi wa mali.


Ndivyo alivyo yeye ajiwekeae nafsi yake akiba wala hawi tajiri machoni pa Mungu.


Bassi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi na ulevi, na masumbufu ya maisha haya,


Nazo zilizoangukia miibani, hawa ndio waliosikia, nao wakienda zao husongwa na shughuli, na mali, na anasa za maisha, wasizae kwa utimilifu.


Hatta Simon alipoona ya kuwa watu wanapewa Roho Mtakatifu kwa kuwekwa mikono ya mitume, akataka kuwapa fedha, akisema,


Wala msifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufunya upya nia zenu, mpate kujua kwa hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Yu wapi mwenye hekima? Yu wapi mwandishi? Yu wapi mleta hoja wa dunia bii? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia liii kuwa upumbavu?


Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa;


ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;


Mtu asijidanganye nafsi yake: kama mtu akijiona kuwa mweuye hekima kati yeuu katika dunia hii, na awe mpumbavu, apate kuwa mwenye hekima.


ambao mungu wa dunia hii amepofusha akili za wasioamini, isiwazukie nuru ya injili ya utukufu wake Kristo aliye sura yake Mungu.


aliyejitoa nafsi yake kwa ajili ya dhambi zetu illi atuokoe na dunia hii mbovu iliyopo sasa, kama alivyopenda Mungu, Baba yetu:


mlizoziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendae kazi sasa katika wana wa kuasi;


Uwaagize walio matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, wala wasitumainie utajiri usio yakini, bali Mungu aliye hayi atupae vitu vyote kwa wingi, tuvitumie kwa furaha;


maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu wa sasa, akasafiri kwenda Thessaloniki; Kreske Galatia, Tito Daimatia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo