Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 12:46 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

46 Alipokuwa katika kusema na makutano, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wakitaka kusema nae.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

46 Yesu alikuwa bado anasema na umati wa watu wakati mama yake na ndugu zake walipofika na kusimama nje, wakitaka kusema naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

46 Yesu alikuwa bado anasema na umati wa watu wakati mama yake na ndugu zake walipofika na kusimama nje, wakitaka kusema naye.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

46 Yesu alikuwa bado anasema na umati wa watu wakati mama yake na ndugu zake walipofika na kusimama nje, wakitaka kusema naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

46 Wakati alikuwa angali anazungumza na umati wa watu, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

46 Wakati alikuwa angali anazungumza na makutano, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye.

Tazama sura Nakili




Mathayo 12:46
26 Marejeleo ya Msalaba  

Na kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipoposwa na Yusuf, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


Mtu akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe.


Huyu si mwana wa sermala? mama yake sio yeye aitwae Mariamu? Na ndugu zake Yakobo, na Yose, na Simon, na Yuda?


Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane.


Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ushike njia kwenda inchi ya Israeli: kwa maana wamekufa walioilafuta roho ya mtoto.


Hakuna mtu ashonae kiraka cha nguo mpya katika vazi kuukuu: ikiwa ashona, kile kipya kilicholiwa huliharibu lile vazi kuukuu, na pale palipolatuka huzidi.


Huyu si yule sermala, mwana wa Mariamu, na ndugu wii Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simon? na ndugu zake wanawake hawapo hapa petu? Wakachukizwa nae.


Na latoka wapi neno hili lililonipata, mama wa Bwana wangu anijilie mimi?


Yusuf na mama yake wakawa wakistaajahu kwa yale yaliyonenwa juu yake;


Sumeon akawabariki, akamwambia Mariamu, mama yake, Hakika huyu amewekwa, waanguke, wasimame wengi katika Israeli; awe ishara inenwayo;


Nao walipomwona wakashangaa sana; mama yake akamwambia, Mwanangu, kwani ukatutenda hivi? Tazama, baba yako na mimi tulikuwa tukikutafuta kwa huzuni.


Akashuka pamoja nao, akafika Nazareti, akawa anawatii: mama yake akayahifadhi maneno haya yote moyoni mwake.


Akasema, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu, bali wengineo kwa mifano, illi wakiona, wasione, na wakisikia, wasitambue.


Na penye msalaba wake Yesu wamesimama mama yake, na ndugu ya mama yake, Mariamu wa Klopa, na Mariamu Magdalene.


NA siku ya tatu palikuwa arusi katika Kana ya Galilaya, na mama yake Yesu alikuwako.


Baada ya haya akashuka hatta Kapernaum, yeye na mama yake na ndugu zake na wanafunzi wake: wakakaa huko siku chache.


Mama yake akawaambia watumishi, Lo lote atakalowaambieni fanyeni.


Hatta ndugu zake walipokwisha kupanda, ndipo yeye nae akapanda kwenda kuishika siku kuu, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.


Bassi ndugu lake wakamwambia, Ondoka bapa uende Yahudi, wanafunzi wako nao wapate kuzitazama kazi zako unazozifanya.


Maana hatta ndugu zake hawakumwamini.


Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kuomba, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama wake Yesu, na ndugu zake.


Hatuna uwezo kuchukua pamoja nasi mke aliye ndugu, kama wao mitume wengine, na ndugu wa Bwana, na Kefa?


Lakini sikumwona mtume mwingine illa Yakobo ndugu yake Bwana.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo