Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 12:45 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

45 Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

45 huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

45 huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

45 huenda kuwachukua pepo wengine saba, wabaya kuliko yeye; na wote huja wakamwingia huyo mtu. Na hali ya mtu huyo sasa huwa mbaya kuliko hapo mwanzo. Ndivyo itakavyokuwa kwa watu hawa waovu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

45 Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kiovu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

45 Kisha huenda na kuwaleta pepo wachafu wengine saba wabaya kuliko yeye mwenyewe, nao huingia na kukaa humo. Nayo hali ya mwisho ya yule mtu huwa ni mbaya kuliko ile ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kiovu.”

Tazama sura Nakili

Mathayo 12:45
23 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini Mafarisayo waliposikia, wakasema, Huyu hafukuzi pepo, illa kwa uweza wa Beelzebul mkuu wa pepo.

Khalafu hunena, Nitarudi nyumbani kwangu nilikotoka; akija, aiona tupu, imefagiwa, na kupambwa.

Lakini namna hii haitoki illa kwa kusali na kufunga.

Ole wenu waandishi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnazunguka katika bahari na inchi kavu illi kumfanya mtu mmoja kuwa mwongofu; na akiisha kufanyika, mnamfanya kuwa mwana wa jehannum marra mbili zaidi kuliko ninyi wenyewe.

Viongozi vipofu, wenye kuchuja mbu na kumeza ngamia.

Alipofufuka Yesu assubuhi siku ya kwanza ya sabato alimtokea kwanza Mariamu Magdalene, ambae kwamba alimtoa pepo saba.

Akamwambia, Jina lako nani? Akajibu, akamwambia, Jina langu Legioni: kwa kuwa tu wengi.

Marra huenda, huchukua pepo saba wengine walio waovu kupita nafsi yake: nao huingia na kukaa humo: na mambo ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza.

Kwa maana shindano letu si juu ya damu na nyama, bali juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza ya ulimwengu huu, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.

Lakini sisi hatumo miongoni mwao wasitao na kupotea, bali miongoni mwao walio na imani ya kutuokoa roho zetu.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo