Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 12:41 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

41 Watu wa Ninawi watasimama siku ile ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nao watakihukumu: maana wao walitubu kwa makhubiri ya Yunus; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Yunus.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

41 Watu wa Ninewi watatokea wakati wa hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Yona!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

41 Watu wa Ninewi watatokea wakati wa hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Yona!

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

41 Watu wa Ninewi watatokea wakati wa hukumu, nao watakihukumu kizazi hiki kwamba kina hatia. Maana Waninewi walitubu kwa sababu ya mahubiri ya Yona, na kumbe hapa kuna kikuu kuliko Yona!

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

41 Siku ya hukumu, watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

41 Siku ya hukumu watu wa Ninawi watasimama pamoja na kizazi hiki na kukihukumu; kwa maana wao walitubu waliposikia mahubiri ya Yona. Na tazama, hapa yupo yeye aliye mkuu kuliko Yona.

Tazama sura Nakili




Mathayo 12:41
20 Marejeleo ya Msalaba  

Akajibu, akawaambia, Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara, wala hakitapewa ishara, ilia ishara ya nabii Yunus.


Malkia wa kusini ataondoka siku ya hukumu pamoja na watu wa kizazi hiki, nae atakihukumu: maana yeye alikuja kutoka pande za mwisho za ulimwengu asikie hekima ya Sulemani; na hapa yupo aliye mkuu kuliko Sulemani.


Marra huenda, akachukua pamoja nae pepo wengine saba walio waovu kupita nafsi yake, nao huingia na kukaa humo; na mambo, ya mwisho ya mtu yule huwa mabaya kuliko ya kwanza. Ndivyo itakavyokuwa kwa kizazi hiki kilicho kiovu.


Lakini nawaambieni, kwamba hapa yupo aliye mkuu kuliko hekalu.


Kizazi kibaya na cha zina chataka ishara; wala hakitapewa ishara, isipokuwa ishara ya nabii Yunus. Akawaacha, akaenda zake.


Yesu akajibu, akasema, Enyi kizazi kisichoamini na kipotofu, nitakuwa pamoja nanyi hatta lini? Nitachukuliana nanyi hatta lini? Mleteni huku kwangu.


Amin, nawaambieni, Mambo haya yote yatakijia kizazi hiki.


Watu wa Ninawi watasimama siku ile ya hukumu pamoja na kizazi hiki, nao wataihukumu: maana wao walitubu kwa ajili ya makhubiri ya Yunus, na hapa pana khabari kubwa kuliko Yunus.


Ajae kutoka juu huyu yu juu ya yote: aliye wa dunia, asili yake ni ya dunia, na anena mambo ya dunia: yeye ajae kutoka mbinguni yu juu ya yote.


Je! wewe u mkubwa kuliko baba yetu Yakobo aliyetupa kisima hiki, nae mwenyewe akanywa maji yake, na wanawe pia, na nyama zake?


Na yeye asiyetahiriwa kwa asili, aishikae torati, hatakuhukumu wewe, uliye na maandiko na kutahiriwa, ukaikhalifu torati?


Kwa imani Nuhu akiisha kuonywa na Mungu khabari za mambo yasiyoonekana bado, kwa kumcha Mungu, aliunda safina, apate kuokoa nyumba yake. Kwa hiyo akauhukumu ulimwengu, akawa mrithi wa haki ipatikanayo kwa imani.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo