Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 12:32 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

32 Na killa mtu atakaenena neno juu ya Mwana wa Adamu atasamehewa, bali yeye atakaenena neno juu ya Roho Mtakatifu hatasamehewa katika ulimwengu wa sasa, wala katika ule ntakaokuwa.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

32 Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

32 Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

32 Tena, asemaye neno la kumpinga Mwana wa Mtu atasamehewa, lakini yule asemaye neno la kumpinga Roho Mtakatifu, hatasamehewa, wala katika ulimwengu huu, wala katika ulimwengu ujao.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

32 Mtu yeyote atakayesema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote anenaye neno dhidi ya Roho wa Mungu hatasamehewa, iwe katika ulimwengu huu au katika ulimwengu ujao.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

32 Mtu yeyote atakayesema neno dhidi ya Mwana wa Adamu atasamehewa, lakini yeyote anenaye neno dhidi ya Roho wa Mwenyezi Mungu hatasamehewa, iwe katika ulimwengu huu au katika ulimwengu ujao.

Tazama sura Nakili




Mathayo 12:32
35 Marejeleo ya Msalaba  

Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake.


Kwa sababu hii nawaambieni, Killa dhambi na killa neno la kufuru watasamehewa wana Adamu, bali kumtukana Roho hawatasamehewa wana Adamu.


Kwa maana Mwana wa Adamu udiye Bwana wa sabato.


Nae aliyepandwa penye miiba, huyu ndiye alisikiae lile neno; na shughuli za dunia, na udanganyifu wa mali hulisonga lile neno, likawa halizai.


na yule adui aliyeyapanda ni shetani; na mavuno ni mwisho wa dunia; na wale wavunao ni malaika.


Bassi, kama vile magugu yakusanywavyo na kuchomwa motoni; ndivyo itakavyokuwa katika mwisho wa dunia hii.


Huyu si mwana wa sermala? mama yake sio yeye aitwae Mariamu? Na ndugu zake Yakobo, na Yose, na Simon, na Yuda?


Yesu akamwambia, Mbweha wana matundu, na ndege za anga vituo; bali Mwana wa Adamu hana pa kulaza kichwa chake.


illa atapewa marra mia sasa wakati huu, nyumba na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na mateso: na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.


Amin, nawaambieni, Dbambi zote watasamehewa wana Adamu, na kufuru zao watakazokufuru zote;


bali mtu atakaemkufuru Roho Mtakatifu hana masamaha hatta milele; bali atakuwa ana dhambi ya milele;


Na killa mmoja atakaesema neno juu ya Mwana wa Adamu, atasamehewa, bali yeye aliyemtukana Roho Mtakatifu hatasamehewa.


Yule bwana akamsifu wakili asiye haki, kwa kuwa alitenda kwa busara: kwa maana wana wa zamani hizi wana busara kuliko wana wa nuru, katika kizazi chao wenyewe.


illa atapokea zaidi marra nyingi sasa wakati huu, na katika ulimwengu ujao uzima wa milele.


Yesu akasema, Baba, uwasamehe, kwa maana hawajui watendalo. Wakagawanya nguo zake, wakipiga kura.


Mwana wa Adamu amekuja, anakula na kunywa, mkasema, Mlafi huyu, na mnywaji wa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi.


Kukawa manungʼuniko mengi katika makutano kwa khabari zake; wengine wakisema, Yu mtu mwema; na wengine wakisema, Sivyo, bali anawadanganya makutano.


Neno hili alilisema katika khabari ya Roho, ambae wale wamwaminio watampokea khalafu: kwa maana Roho Mtakatifu alikuwa bado kuwapo, kwa sababu Yesu alikuwa bado kutukuzwa.


Wakajibu, wakamwambia, Wewe nawe umetoka Galilaya? Tafuta, ukaone ya kuwa kutoka Galilaya hakutokea nabii.


Tubuni bassi, mrejee, illi dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuhurudishwa kwa kuwako kwake Bwana:


juu sana kuliko ufalme wote, na mamlaka, na nguvu, na usultani, na killa jina litajwalo, si ulimwenguni humu tu, bali katika ule ujao nao;


mimi niliyekuwa kwanza mtukanaji, mwenye kuudhi watu, mwenye jeuri: lakini nalirehemiwa kwa kuwa nalitenda hivyo kwa njinga, na kwa kutokuwa na imani;


Ni neno la kuaminiwa, listahililo kukubaliwa na watu wote, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni, awaokoe wenye dhambi; na mimi wa kwanza wao.


Jitahidi kupata utawa. Maana, kujitahidi kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, hali utawa hufaa kwa mambo yote; maana nna ahadi ya uzima wa sasa na wa ule utakaokuwa.


Uwaagize walio matajiri katika ulimwengu huu wasijivune, wala wasitumainie utajiri usio yakini, bali Mungu aliye hayi atupae vitu vyote kwa wingi, tuvitumie kwa furaha;


maana Dema aliniacha, akiupenda ulimwengu wa sasa, akasafiri kwenda Thessaloniki; Kreske Galatia, Tito Daimatia.


yatufundisha kukataa ubaya na tamaa za kidunia, ua kuishi kwa kiasi, na haki, na utawa, katika ulimwengu wa sasa,


Dini iliyo safi na isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika shidda yao, na kujilinda pasipo mawaa katika dunia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo