Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 12:29 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

29 Ama awezaje mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuviteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? ndipo atakapoiteka nyumba yake.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

29 “Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyanganya mali yake, bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenye nguvu? Hapo ndipo atakapoweza kumnyanganya mali yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

29 “Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyanganya mali yake, bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenye nguvu? Hapo ndipo atakapoweza kumnyanganya mali yake.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

29 “Au, anawezaje mtu kuivamia nyumba ya mtu mwenye nguvu na kumnyang'anya mali yake, bila kwanza kumfunga huyo mtu mwenye nguvu? Hapo ndipo atakapoweza kumnyang'anya mali yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

29 “Au tena, mtu anawezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali yake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akishamfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali yake.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

29 “Au tena, mtu awezaje kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuteka nyara mali zake asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu? Akishamfunga, ndipo hakika anaweza kuteka nyara mali zake.

Tazama sura Nakili




Mathayo 12:29
11 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini mimi nikifukuza pepo kwa uweza wa Bobo ya Mungu, bassi ufalme wa Mungu umekujieni.


Mtu asiye upande wangu yu kinyume changu; na mtu asivekusanya pamoja nami hutapanya.


Hawezi mtu kuingia ndani ya nyumba ya mtu mwenye nguvu, na kuteka vyombo vyake, asipomfunga kwanza yule mwenye nguvu; ndipo atakapoiteka nyumba yake.


afanyae dhambi yu wa Shetani: kwa kuwa Shetani hutenda dhambi tangu mwanzo. Kwa kusudi hili Mwana wa Mungu alidhihiri, illi azivunje kazi za Shetani.


Ninyi, watoto wangu, mwatokana na Mungu: nanyi mmewashinda, kwa sababu yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika dunia.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo