Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 12:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Nae Yesu akijua haya akatoka huko: makutano mengi wakamfuata; akawaponya wote,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Lakini Yesu alipojua jambo hilo, akatoka mahali pale. Watu wengi walimfuata, akawaponya wagonjwa wote,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Lakini Yesu alipojua jambo hilo, akatoka mahali pale. Watu wengi walimfuata, akawaponya wagonjwa wote,

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Lakini Yesu alipojua jambo hilo, akatoka mahali pale. Watu wengi walimfuata, akawaponya wagonjwa wote,

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Lakini Isa alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi walimfuata, naye akawaponya wote waliokuwa wagonjwa miongoni mwao,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Lakini Isa alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi wakamfuata, naye akawaponya wagonjwa wao wote,

Tazama sura Nakili




Mathayo 12:15
15 Marejeleo ya Msalaba  

Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine: kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza miji yote ya Israeli, hatta ajapo Mwana wa Adamu.


Makutano mengi wakamfuata, akawaponya huko.


Na killa alikokwenda, akiingia vijijini, au mijini, au mashambani, wakawaweka wagonjwa sokoni, wakamsihi waguse walao upindo wa vazi lake: nao wote waliomgusa wakapona.


Yesu akafahamu fikara zao akajibu, akawaambia, Mnafikiri nini mioyoni mwenu?


Ikawa katika siku zile akaomloka akaenda mlimani kuomba, akashinda usiku kucha, akimwomba Mungu.


Namakutano walipojua wakamfuata: akawakaribisha, akanena nao khabari za ufalme wa Mungu, akawaponya waliokuwa na haja ya kuponywa.


Bassi Yesu hakutemhea tena kwa wazi kati ya Wayahudi, hali alitoka huko akaenda mahali karibu ya jangwa, hatta mji nitwao Efraim; akakaa huko pamoja na wanafunzi wake.


NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.


Yanipasa kuzifanya kazi zake aliyenipeleka maadam ni mchana: usiku waja, asipoweza mtu kufanya kazi.


Na tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia.


Kwa sababu ndio mlioitiwa: maana Kristo nae aliteswa kwa ajili yenu, akiwaachieni mfano, mfuate nyayo zake;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo