Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 11:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Nawe Kapernaum, uliyeinuliwa hatta mbinguni, utashushwa hatta kuzimu: kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwako, ingalifanyika katika Sodom, ungalikuwapo hatta leo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 Na wewe Kafarnaumu, je, utajikweza mpaka mbinguni? Utaporomoshwa mpaka kuzimu! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwako ingalifanyika kule Sodoma, mji huo ungalikuwako mpaka hivi leo.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha! Utashushwa hadi Kuzimu. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungekuwepo hadi leo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Nawe Kapernaumu, je, utainuliwa hadi mbinguni? La hasha, utashushwa mpaka kuzimu. Miujiza iliyofanyika kwako ingefanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwepo hadi leo.

Tazama sura Nakili




Mathayo 11:23
30 Marejeleo ya Msalaba  

Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule.


Nami nakuambia, Wewe ndiwe Petro, na jun ya mwamba huu nitalijenga kanisa langu; na milango ya kuzimu haitalishinda.


Hatta walipofika Kapernaum, wale watozao nussu shekeli wakamwendea Petro, wakasema, Je! Mwalimu wenu hatoi nussu shekeli?


akatoka Nazareti, akaenda, akakaa Kapernaum, ulioko pwani, mipakani mwa Zabulon na Nafthalim:


Hatta Yesu alipoingia Kapernaum, akida alimjia, akamsihi,


Nawe Kapernaum, wewe uliyeinuliwa hatta mhinguni, ntashushwa hatta kuzimu.


Kwa maana killa ajikwezae atadhilika; nae ajidhiliye atakwezwa.


Bassi katika akhera akainua macho yake, akiwa katika adhabu, akamwona Ibrahimu yuko mbali, na Lazaro kifuani pake.


Akawaambia, Hapana shaka mtaniambia methali hii, Tabibu, jiponye nafsi yako: mambo yote tuliyosikia yametendeka Kapernaum, yatende na hapa pia katika inchi yako mwenyewe.


Kwa maana hutaniacha roho yangu katika kuzimu: Wala hutamtoa Mtakatifu wako aone uharibifu.


akitangulia kuyaona haya, alitaja khabari za kufufuka kwake Kristo, ya kama roho yake haikuachwa katika kuzimu, wala mwili wake hankuona uharibifu,


Kama vile bodoma na Gomora, na miji iliyozunguka, waliofuata uasharati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wamepasiwa hukumu yamoto wa milele.


na aliye hayi; nami nalikuwa nimekufa, na tazama ni hayi hatta milele na milele. Amin. Nami ninazo funguo za mauti, na za kuzimu.


Na mizoga yao itakuwa katika njia ya mji ule mkuu uitwao kwa jinsi ya roho Sodoma, na Misri, tena ni hapo Bwana wetu aliposulibiwa.


Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao.


Nikaona, na tazama, farasi wa rangi ya kijivujivu, na yeye aliyempanda jina lake ni Manti, na Kuzimu akafuatana nae. Wakapewa mamlaka juu ya robo ya inchi wane kwa upanga na kwa njaa na kwa tauni na kwa nyama mwitu wa inchi.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo