Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 11:21 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

21 Ole wako, Korazin! Ole wako, Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika katika Turo na Sidon, wangalitubu zamani kwa kuvaa gunia na majivu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

21 “Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia kitambo na kujipaka majivu kutubu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

21 “Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia kitambo na kujipaka majivu kutubu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

21 “Ole wako Korazini! Ole wako Bethsaida! Maana, kama miujiza iliyofanyika kwenu ingalifanyika kule Tiro na Sidoni, watu wake wangalikwisha vaa mavazi ya gunia kitambo na kujipaka majivu kutubu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

21 “Ole wako, Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

21 “Ole wako, Korazini! Ole wako Bethsaida! Kwa maana kama miujiza iliyofanyika kwenu, ingefanyika Tiro na Sidoni, miji hiyo ingekuwa imetubu zamani kwa kuvaa magunia na kujipaka majivu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 11:21
31 Marejeleo ya Msalaba  

Lakini, nawaambieni, itakuwa rakhisi Turo na Sidon istahimili adhabu zao siku ya hukumu kuliko ninyi.


Yesu akatoka huko, akaenda pande za Turo na Sidon.


Ole wa ulimwengu kwa sababu ya mambo ya kukosesha! Maana hayana buddi kuja mambo ya kukosesha; lakini ole wake mtu yule aliletae jambo la kukosesha!


Mwana wa Adamu aenda zake, kama alivyoandikiwa: lakini ole wake mtu yule ambae Mwana wa Adamu anasalitiwa nae! Ingekuwa kheri kwake mtu yule kama asingalizaliwa.


na toka Idumaya, na ngʼambu ya Yardani, na pande za Turo na Sidon, mkutano mkuu, waliposikia khabari za mambo yote aliyokuwa akiyatenda; wakamwendea.


Marra akawashurutisha wanafunzi wake wapande chomboni, watangulie kwenda ngʼambu hatta Betsaida wakati yeye alipokuwa akiwaaga makutano.


Akaondoka huko, akaenda zake hatta mipaka ya Turo na Sidon. Akaingia katika nyumba, akataka isijulikane na mtu; lakini hakuweza kustirika.


Akatoka tena katika mipaka ya Turo akapita katikati ya Sidon, akaenda hatta bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Dekapoli.


Wakalika Bethsaida, wakamletea kipofu, wakamsihi amguse.


wala hakutumwa Eliya kwa mmojawapo wao, illa kwa mjane mmoja wa Sarepta, mji wa Sidon.


Akatelemka pamoja nao, akasimama panapo uwanda, pamoja na kundi la wanafunzi wake, na kundi la watu waliotoka Yahudi wote, na Yerusalemi, na pwani ya Turo na Sidon, waliokuja wamsikilize na kuponywa maradhi zao;


Wale mitume waliporudi wakamweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda zake kwa faragha mahali pasipo watu, karibu na mji uitwao Bethsaida.


Nae Filipo alikuwa mtu wa Bethsaida, mtu wa mji wa Andrea na Petro.


Bassi hao walimwendea Filipo wa Bethsaida wa Galilaya, wakimwuliza, wakisema, Bwana, tunataka kumwona Yesu.


Nae Herode aliwakasirikia sana watu wa Tʼuro na Sidon: wakamwendea kwa nia moja, na wakiislia kufanya urafiki na Blasto, mwenye kukitunza chumba cha mfalme cha kulalia, wakataka amani; kwa maana inchi yao ilipata riziki kwa inchi ya mfalme.


Siku ya pili tukawasili Sidon; Yulio akamfadhili sana Paolo akampa rukhusa kwenda kwa rafiki zake, kutunzwa nao.


Ole wao! kwa sababu walikwenda katika njia ya Kain, na kulifuata kosa la Balaam pasipo kujizuia, kwa ajili ya ujira, nao wameangamia katika maasi ya Kora.


Nami nitawarukhusu mashahidi wangu wawili, nao watatoa unabii siku elfu na miateen na sittini, wamevikwa mavazi ya kigunia.


Nikaona, alipoifungua muhuri ya sita, tazama, palikuwa tetemeko kuu la inchi, jua likawa jeusi kama gunia la nywele, mwezi ukawa kama damu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo