Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 11:19 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

19 Mwana wa Adamu alikuja, akila na kunywa, wakanena, Mlafi huyu, na mnywa mvinyo, rafiki wa watoza ushuru na wenye dhambi! Na hekima imepewa haki na watoto wake.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

19 Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: ‘Mwangalieni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watozaushuru na wenye dhambi!’ Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

19 Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: ‘Mwangalieni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watozaushuru na wenye dhambi!’ Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

19 Mwana wa Mtu akaja, anakula na kunywa, nao wakasema: ‘Mwangalieni huyu, mlafi na mlevi, rafiki yao watozaushuru na wenye dhambi!’ Hata hivyo, hekima ya Mungu inathibitishwa kuwa njema kutokana na matendo yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

19 Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

19 Mwana wa Adamu alikuja akila na kunywa, nao wanasema, ‘Tazameni huyu mlafi na mlevi, rafiki wa watoza ushuru na “wenye dhambi.” ’ Lakini hekima huthibitishwa kuwa kweli kwa matendo yake.”

Tazama sura Nakili

Mathayo 11:19
19 Marejeleo ya Msalaba  

Maana mkiwapenda wanaowapendani, mwapata thawabu gani? Hatta watoza ushuru, je, nao hawafanyi yayo hayo?

IKAWA, Yesu alipoingia katika nyumba ya mtu mmoja, mtu mkuu katika Mafarisayo, siku ya sabato, ale chakula, walikuwa wakimvizia.

Hatta watu walipoona wakanungʼunika wote, wakisema, ya kama, Ameingia akae kwa mtu mwenye dhambi.

Watu wote na watoza ushuru waliposikia wakampa Mungu haki, kwa kuwa wamebatizwa kwa ubatizo wa Yohana.

Yesu nae akaitwa pamoja na wanafunzi wake arusini.

Killa mtu miongoni mwetu ampendeze jirani yake apate wema akajengwe.

wakisema, Amin: Baraka na utukufu na hekima na shukrani na heshima na uweza na nguvu zina Mungu wetu milele na milele. Amin.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo