Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 10:7 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

7 Na katika kuenenda kwenu, khubirini, nikinena, Ufalme wa mbinguni umekaribia.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

7 Mnapokwenda hubirini hivi: ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

7 Mnapokwenda hubirini hivi: ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

7 Mnapokwenda hubirini hivi: ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

7 Mnapoenda, hubirini ujumbe huu, ‘Ufalme wa mbinguni umekaribia.’

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

7 Wakati mnapokwenda, hubirini mkisema, ‘Ufalme wa Mbinguni umekaribia.’

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:7
19 Marejeleo ya Msalaba  

Ponyeni wagonjwa, takaseni wenye ukoma, fufueni wafu, fukuzeni pepo; mmepata burre, toeni burre.


IKAWA Yesu alijiokwisha kuwaagiza wanafunzi wake thenashara, akatoka huka kwenda kufundisha na kukhubiri katika miji yao.


Katika hawa wawili ni yupi aliyefanya mapenzi ya baba yake? Wakamwambia, Yule wa kwanza. Yesu akawaambia, Amin, nawaambieni, watoza ushuru na makahaba wanatangulia mbele yenu kuingia katika ufalme wa Mungu.


Kwa sababu hii nawaambieni, ya kwamba ufalme wa Mungu utaondolewa kwenu, na watapewa taifa lingine wenye kuzaa matunda yake.


Ole wenu waandisbi na Mafarisayo, wanafiki! kwa kuwa mnakula nyumba za wajane, na kwa unafiki mnasali sala ndefu; kwa hiyo mtapokea hukumu iliyo kubwa mno.


Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Tokea wakati huo Yesu akaanza kukhubiri, na kusema, Tubuni, maana ufalme wa mbinguni umekaribia.


Wakatoka, wakakhubiri kwamba watu watubu.


Torati na manabii zilikuwako mpaka Yohana. Tangu wakati ule, khabari njema ya ufalme wa Mungu inakhubiriwa, na killa mtu anauingia kwa nguvu.


Akawatuma kuukhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.


Wakaenda zao, wakazunguka katika vijiji, wakiikhubiri injili, na kuponya watu killa pahali.


Akamwambia, Waache wafu wazike wafu wao, bali wewe enenda zako ukautangaze ufalme wa Mungu.


huyu alikuja kwa Yesu usiku, akamwambia, Rabbi, twajua ya kuwa u mwalimu, umetoka kwa Mungu; kwa maana hakuna mtu awezae kuzifanya ishara hizi uzifanyazo wewe, illa Mungu awe pamoja nae.


Petro alipokuwa akiingia, Kornelio akatoka amlaki akamwangukia miguu, akamsujudia.


wakifadhaika sana kwa sababu wanawafundisha watu na kuukhubiri ufufuo wa wafu unaopatikana kwa Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo