Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 10:5 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

5 Hawa thenashara Yesu aliwatuma, akawaagiza, akinena, Katika njia ya Mataifa msiende, wala mjini mwa Wasamaria msiingie:

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

5 Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika miji ya Wasamaria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

5 Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika miji ya Wasamaria.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

5 Yesu aliwatuma hao kumi na wawili na kuwapa maagizo haya: “Msiende kwa watu wa mataifa mengine, wala msiingie katika miji ya Wasamaria.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

5 Hawa kumi na wawili, Isa aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

5 Hawa kumi na wawili, Isa aliwatuma akawaagiza: “Msiende miongoni mwa watu wa Mataifa, wala msiingie mji wowote wa Wasamaria.

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:5
27 Marejeleo ya Msalaba  

Akawatuma watumishi wake wawaite walioalikwa kuja arusini: nao hawakutaka kuja.


Inchi ya Zabulon na inchi ya Nafthalim, Njia ya bahari ngʼambu ya Yordani, Galilaya ya mataifa,


Akawaita wale thenashara, akaanza kuwatuma wawili wawili; akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu:


BASSI baada ya mambo haya Bwana akachagua wengine sabaini, akawatuma wawili wawili wamtangulie kwenda killa mji na pahali atakakokwenda mwenyewe.


Lakini Msamaria mmoja akisafiri, akamjia, nae alipomwona akamhurumia;


akaanguka kufudifudi miguuni pake, akimshukuru; nae ni Msamaria.


AKAWAITA wale thenashara akawapa uweza na mamlaka juu ya pepo wote, na kuponya maradhi.


Akawatuma kuukhubiri ufalme wa Mungu na kuponya wagonjwa.


Kama ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo hivyo naliwatuma wao ulimwenguni.


Bassi Yesu akawaambia marra ya pili, Amani kwenu; kama Baba alivyonipeleka, nami nawatuma ninyi.


Baba zetu waliabudu katika mlima huu, na ninyi husema kwamba Yerusalemi ni mahali patupasapo kuabudia.


Bassi akafika mji wa Samaria, uitwao Sukar, karibu na lile shamba ambalo Yakobo alimpa Yusuf mwanawe.


Bassi yule mwanamke wa Kisamaria akamwambia, Imekuwaje wewe Myahudi kutaka maji kwangu, nami ni mwanamke wa Kisamaria? kwa maana Wayahudi hawachangamani na Wasamaria.


Bassi Wayahudi wakasemezana wao kwa wao, Huyu atakwenda wapi hatta sisi tusimwone? Atakwenda kwa Utawauyiko wa Wayunani na kuwafundisha Wayunani?


Wayahudi wakajibu wakamwambia, Hatuneni vema sisi kwamba wewe u Msamaria, na una pepo?


Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi.


Na wale waliotahiriwa walioamini, wakashangaa, watu wote waliokuja pamoja na Petro, kwa sababu mataifa nao wameshukiwa kipaji cha Roho Mtakatifu.


NA Saul alikuwa akiona vema auawe. Siku ile kukatukia adha nyingi juu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wote wakatawanyika katika inchi ya Yahudi na Samaria, illa mitume.


wakituzuia tusiseme na mataifa wapate kuokolewa; illi watimize dhambi zao siku zote; lakini hasira imewafikia hatta mwisho.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo