Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 10:4 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

4 Simon Kananayo, na Yuda Iskariote, ndiye aliyemsaliti.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

4 Simoni Mkanaani, na Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

4 Simoni Mkanaani, na Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

4 Simoni Mkanaani, na Yuda Iskarioti ambaye alimsaliti Yesu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

4 Simoni Mkananayo, na Yuda Iskariote aliyemsaliti Isa.

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:4
19 Marejeleo ya Msalaba  

Kisha mmoja wa wale thenashara, jina lake Yuda Iskariote, alikwenda zake kwa makuhani wakuu,


akasema, Nini mtakayonipa, nami nitamsaliti kwenu? Wakampimia vijiande thelathini vya fedha.


Mwajua ya kuwa baada ya siku mbili itakuwa pasaka, na Mwana wa Adamu atasalitiwa apate kusulibiwa.


Hatta alipokuwa akisema, Yuda, mmoja wa wale thenashara akaja, na pamoja nae makutano mengi, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu na wazee wa watu.


Ndipo Yuda, yule mwenye kumsaliti, alipoona ya kuwa amekwisha kuhukumiwa, akajuta, akawarudishia makuhani wakuu na wazee vile vipande thelathini vya fedha,


Yuda Iskariote, mmoja wa wathenashara, akaenda zake kwa makuhani wakuu, apate kumsaliti kwao.


Na alipokuwa katika kusema marra Yuda akafika, mmoja wa wathenashara, na pamoja nae mkutano, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu, na waandishi, na wazee.


Shetani akamwingia Yuda, aitwae Iskariote, nae alikuwa katika hesabu ya wale thenashara.


Nae alipokuwa akisema, tazama, makutano, nae aitwae Yuda, mmoja wa wathenashara, akitangulia mbele yao, akamkaribia Yesu kumbusu.


Hatta wakati wa chakula cha jioni, Shetani alipokwisha kumtia Yuda, mwana wa Simon Iskariote, moyo wa kumsaliti,


Lakini kuna wengine miongoni mwemi wasioamini. Maana Yesu alijua tangu mwanzo ni nani wasioamini na ni nani atakaenisaliti.


Alimnena Yuda, mwana wa Simon Iskariote: maana huyu ndiye atakaemsaliti: nae ni mmoja wa wathenashara.


Hatta walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartolomayo na Mattayo, Yakobo wa Alfayo, na Simon Zelote, na Yuda wa Yakobo.


atwae sehemu yake ya khuduma hii na utume huu, alioukosa Yuda aende zake mahali pake.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo