Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 10:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Niwaambialo ninyi katika giza, lisemeni kalika nuru; na msikialo kwa siri, likhubirini juu ya nyumba.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Ninalowaambieni nyinyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinongonezwa, litangazeni hadharani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Ninalowaambieni nyinyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinongonezwa, litangazeni hadharani.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Ninalowaambieni nyinyi katika giza, lisemeni katika mwanga; na jambo mlilosikia likinong'onezwa, litangazeni hadharani.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe. Na lile mnalosikia likinong’onwa masikioni mwenu, lihubirini juu ya nyumba.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Ninalowaambia gizani, ninyi lisemeni mchana peupe. Na lile mnalosikia likinong’onwa masikioni mwenu, lihubirini juu ya nyumba.

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:27
16 Marejeleo ya Msalaba  

nae aliye juu ya nyumba asishuke avichukue vitu vilivyomo nyumbani mwake;


Bassi yo yote mliyoyasema gizani, yatasikiwa katika nuru: nalo mlilolisema katika sikio la mtu katika vyumba vya ndani litakhubiriwa juu darini.


Akasema, Ninyi mmejaliwa kuzijua siri za ufalme wa Mungu, bali wengineo kwa mifano, illi wakiona, wasione, na wakisikia, wasitambue.


MANENO haya nimewaambieni msije mkachukizwa.


Lakini ajapo yeye, Roho ya kweli, atawaongozeni katika yote iliyo kweli: kwa maana hatasema kwa shauri lake yeye, lakini yote atakayosikia, atayasema, na mambo yajayo atawapasha khabari yake.


Haya nimesema nanyi kwa methali: saa inakuja, sitasema nanyi tena kwa methali, lakini nitawapa kwa wazi khabari ya Baba.


Wanafunzi wake wakasema, Tazama, sasa wasema waziwazi, wala huneni methali yo yote.


Bassi katika sunagogi akahujiana na Wayahudi nao waliomcha Mungu, na killa siku sokoni na wale waliokutana nae.


Enendeni mkasimame hekaluni mkawaambie watu maneno yote ya uzima huu.


Je! hatukuwaamuru ninyi kwa nguvu, msifundishe kwa jina hili: nanyi mmeijaza Yerusalemi mafundisho yenu, na mnataka kuleta damu ya mtu yule juu yetu.


Bassi, kwa kuwa tuna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo