Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 10:23 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

23 Watakapowaudhi katika mji huu, kimbilieni mwingine: kwa maana ni kweli nawaambieni, Hamtaimaliza miji yote ya Israeli, hatta ajapo Mwana wa Adamu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

23 “Watu wakiwadhulumu katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kweli nawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katika miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Mtu hajafika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

23 “Watu wakiwadhulumu katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kweli nawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katika miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Mtu hajafika.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

23 “Watu wakiwadhulumu katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Kweli nawaambieni, hamtamaliza ziara yenu katika miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Mtu hajafika.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

23 Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu kuja.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

23 Wakiwatesa katika mji mmoja, kimbilieni mji mwingine. Amin, amin nawaambia, hamtamaliza miji yote ya Israeli kabla Mwana wa Adamu kuja.

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:23
29 Marejeleo ya Msalaba  

Kwa maana Mwana wa Adamu atakuja katika utukufu wa Baba yake pamoja na malaika zake; ndipo atamlipa killa mtu kwa kadiri ya kutenda kwake.


Amin, nawaambieni, Pana watu katika hawo wanaosimama hapa, ambao hawataonja mauti kabisa, hatta watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika ufalme wake.


Na hawo walipokwisha kwenda zao, malaika wu Bwami akamtokea Yusuf katika ndoto, akiuena, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukakae huko mpaka nikuambiapo; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.


Kwa sababu hii, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi: na wengine wao mtawaua na mtawasulibi, na wengine wao mtawapiga katika sunagogi zenu, na mtawafukuza mji kwa mji;


Amin, nawaambieni, Mambo haya yote yatakijia kizazi hiki.


Kwa maana kama vile umeme utokavyo mashariki ukaonekana hatta magharibi; hivyo ndivyo kutakavyokuwa kuja kwake Mwana wa Adamu.


ndipo itakapoonekana ishara yake Mwana wa Adamu mbinguni: ndipo mataifa yote ya ulimwengu wataomboleza, nao watamwona Mwana wa Adamu akija juu ya mawingu ya mbingu kwa nguvu pamoja na utukufu mwingi.


Amin, nawaambieni, Hakitapita kizazi hiki, hatta yatakapokuwa haya yote.


Bali mtumishi yule mbaya akisema moyoni mwake, Bwana wangu anakawia;


Bassi kesheni, maana hamwijui siku wala saa ajapo Mwana wa Adamu.


Yesu akamwambia. Wewe umesema: lakini nawaambieni, Tangu sasa mtamwoua Mwana wa Adamu ameketi mkono wa kuume wa nguvu, akija juu ya mawingu.


Yesu aliposikia ya kwamba Yohana amefungwa, akaenda zake hatta Galilaya;


Hapo ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija mawinguni pamoja na nguvu nyingi na utukufu.


Walakini Mwana wa Adamu atakapokuja, je! ataiona imani duniani?


Ndipo watakapomwona Mwana wa Adamu akija katika wingu kwa nguvu na utukufu mwingi.


NA baada ya haya Yesu akawa akitembea katika Galilaya: maana hakutaka kutembea katika Yahudi, kwa sababu Wayahudi walikuwa wakitafuta kumwua.


Marra ndugu wakawapeleka Paolo na Sila usiku hatta Beroya. Walipofika huko wakaingia katika sunagogi la Wayahudi.


Marra hiyo wale ndugu wakampeleka Paolo aende zake kana kwamba anakwenda njia ya pwani; bali Sila na Timotheo wakashinda huko.


KISHINDO kile kilipokoma, Paolo akawaita wanafunzi akaagana nao, akaondoka aende zake hatta Makedonia.


NA Saul alikuwa akiona vema auawe. Siku ile kukatukia adha nyingi juu ya kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wote wakatawanyika katika inchi ya Yahudi na Samaria, illa mitume.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo