Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 10:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 Na majina ya mitume thenashara ni haya: Wa kwanza Simon aliyekwitwa Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake;

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 Majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya: Wa kwanza ni Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohane ndugu yake;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 Majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya: Wa kwanza ni Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohane ndugu yake;

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 Majina ya hao mitume kumi na wawili ni haya: wa kwanza ni Simoni aitwaye Petro, na Andrea ndugu yake; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohane ndugu yake;

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili: wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye;

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 Haya ndiyo majina ya hao mitume kumi na wawili: wa kwanza, Simoni aitwaye Petro, na Andrea nduguye; Yakobo mwana wa Zebedayo, na Yohana nduguye;

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:2
44 Marejeleo ya Msalaba  

NA baada ya siku sita Yesu akawachukua Petro, na Yakobo, na Yohana ndugu yake, akawaleta juu ya mlima mrefu peke yao;


Ndipo mama ya wana wa Zebedayo akamwendea pamoja na wanawe, akimsujudia, akimwomba neno.


Akamchukua Petro na wana wawili wa Zebedayo, akaanza kufadhaika, na kuhuzunika moyo.


Nae Yesu akitembea kando ya bahari ya Galilaya, akaona ndugu wawili, Simon aitwae Petro, na Andrea ndugu yake, wakitupa jarife baharini; maana walikuwa wavuvi.


Akaendelea mbele, akaona ndugu wengine wawili. Yakob wa Zebedayo, na Yohana ndugu yake, walikuwa katika chombo pamoja na Zebedayo baba yao, wakitengeneza nyavu zao; akawaita.


Marra walipotoka katika sunagogi, wakalika nyumbani kwa Simon na Andrea, pamoja na Yakobo na Yohana.


Hatta alipokuwa ameketi katika mlima wa mizeituni, kuelekea hekalu, Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea wakamwuliza kwa faragha, Tuambie, haya yatakuwa lini?


Na mitume wakakusanyika mbele ya Yesu; wakampa khabari za mambo yote waliyoyafanya na mambo yote waliyoyafundisha.


Na kwa hiyo hekima ya Mungu ilisema, Nitatuma kwao manabii na mitume, na wataua baadhi yao, na kuwaudhi,


Bassi saa ilipowadia, akaketi, na mitume pamoja nae.


Akapeleka Petro na Yohana, akisema, Enendeni, mkatuandikie pasaka, illi tuile.


Kadhalika Yakobo na Yohana, wana wa Zebedayo, waliokuwa washiriki wa Simon, Yesu akamwambia Simon, Usiogope; tangu sasa utakuwa ukivua watu.


Wale mitume waliporudi wakamweleza mambo yote waliyoyatenda; akawachukua, akaenda zake kwa faragha mahali pasipo watu, karibu na mji uitwao Bethsaida.


Filipo akaenda, akamwambia Andrea; kiisha Andrea na Filipo wakamwambia Yesu.


Palikuwako mmoja wa wanafunzi wake, amemwegamia Yesu kifua chake, ambae Yesu alimpenda.


Bassi akaenda mbio hatta kwa Simon Petro, na kwa mwanafunzi yule mwingine aliyependwa na Yesu, akawaambia, Wamemwondoa Bwana kaburini, wala hatujui walikomweka.


Simon Petro, na Tomaso aitwae Didumo, na Nathanael wa Kana wa Galilaya, na wana wa Zebedayo, na watu wengine wawili katika wanafunzi wake, walikuwa mahali pamoja.


Na Petro akigeuka, akamwona mwanafunzi yule aliyependwa na Yesu akifuata; yeye ndiye aliyeegamia kifuani pake wakati wa kula chakula cha jioni na kusema, Bwana yu nani akusalitiye?


Huyu ndiye mwanafunzi ayashuhudiae haya, na aliyeandika haya; na twajua ya kuwa ushuhuda wake ni wa kweli.


Bassi Yesu akawaambia wathenashara, Ninyi nanyi mnataka kuondoka?


Yesu akawajibu, Je! sikuwachagua ninyi thenashara, na mmoja wenu ni Shetani?


Alimnena Yuda, mwana wa Simon Iskariote: maana huyu ndiye atakaemsaliti: nae ni mmoja wa wathenashara.


Mmoja wa wanafunzi wake, Andrea, ndugu wa Simon Petro, akamwambia,


Hatta walipoingia, wakapanda orofani, walipokuwa wakikaa; Petro, na Yakobo, na Yohana, na Andrea, Filipo na Tomaso, Bartolomayo na Mattayo, Yakobo wa Alfayo, na Simon Zelote, na Yuda wa Yakobo.


Wakawapigia kura: kura ikamtoa Mattiya; akachaguliwa kuwa pamoja na mitume edashara.


Akamwua Yakobo ndugu wa Yohana kwa upauga.


BASSI Petro na Yohana walikuwa wakipanda pamoja kwenda hekaluni, saa ya kusali, saa tissa.


baadae alionekana na Yakobo; tena na mitume wote;


Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu,


KWA hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki wito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu,


PETRO, mtume wa Yesu Kristo, kwa wateule wa Mtawanyiko, wakaao bali ya wageni katika Ponto, Galatia, Kappadokia, Asia na Bithunia,


SIMON PETRO, mtumwa na mtume wa Yesu m Kristo, kwao waiiopata imani moja na sisi, yenye thamani, katika haki ya Mungu wetu, na Mwokozi wetu Yesu Kristo.


MZEE kwa bibi mteule na watoto wake niwapendao katika kweli; wala si mimi peke yangu, bali na ndugu wote waijuao ile kweli;


MZEE kwa Gaio mpenzi, nimpendae katika kweli.


UFUNUO wa Yesu Kristo aliopewa na Mungu awaonyeshe watumishi wake mambo ambayo kwamba hayana buddi kuwa upesi: akatuma kwa mkono wa malaika akamwonyesha mtumishi wake Yohana;


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Furahini juu yake, enyi mbingu, na ninyi watakatifu na mitume na manabii, kwa maana Mungu amehukumu hukumu yenu juu yake.


Na mimi Yohana ndimi niliye mwenye kuona haya na kuyasikia. Na niliposikia na kuyaona nalianguka nisujudu mbele ya miguu ya malaika yule mwenye kunionyesha haya.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo