Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 10:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Amin, nawaambieni, Itakuwa rakhisi inchi ya Sodoma na Gomora istahimili adhabu yao siku ya hukumu, kuliko mji ule.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Kweli nawaambieni, siku ya hukumu mji huo utapata adhabu kubwa kuliko ile iliyoipata miji ya Sodoma na Gomora.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Kweli nawaambieni, siku ya hukumu mji huo utapata adhabu kubwa kuliko ile iliyoipata miji ya Sodoma na Gomora.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Kweli nawaambieni, siku ya hukumu mji huo utapata adhabu kubwa kuliko ile iliyoipata miji ya Sodoma na Gomora.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa miji ya Sodoma na Gomora kustahimili katika hukumu kuliko mji huo.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Amin, nawaambia, itakuwa rahisi zaidi kwa miji ya Sodoma na Gomora kustahimili katika hukumu kuliko mji huo.

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:15
22 Marejeleo ya Msalaba  

Bassi, nawaambieni, Killa neno lisilo maana, watakalolisema wana Adamu, watatoa hesabu ya neno hilo siku ya hukumu.


Kwa maana, amin nawaambieni, Mpaka mbingu na inchi zitakapoondoka, yodi moja na nukta moja ya torati haitaondoka, mpaka yote yatimie.


Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kufukuza pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?


Na watu wote wasiokaribisha ninyi wala kuwasikia, mtokapo huko, yakungʼuteni mavumbi yaliyo chini ya miguu yenu kuwa ushuhuda kwao.


Anikataae mimi, asiyekubali maneno yangu, anae amhukumuye: neno lile nililolisema, ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.


Na mapenzi yake Baba aliyenipeleka ni haya, ya kwamba katika vyote alivyonipa nisipoteze kitu hatta kimoja, hali nikifufue siku ya mwisho.


Na mapenzi yake aliyenipeleka ni haya ya kwamba killa amtazamae Mwana na kumwamini awe ua uzima wa milele, nami nitamfufua siku ya mwisho.


Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.


kazi ya killa mtu itakuwa dhahiri. Maana siku ile itaidhihirisha, kwa kuwa yafunuliwa katika moto; na ule moto utajaribu kazi ya killa mtu, ni wa namna gani.


Bali ninyi, ndugu, hamwi katika giza, siku ile iwapale kama mwizi.


tusiache kukusanyika pamoja, kama ilivyo desturi ya wengine; bali tukionyana; na tukizidi, kwa kadiri mwonavyo siku ile kuwa inakaribia.


akaihukumu miji ya Sodoma na Gomora, akiipiudua ua kuifanya majivu, akaifanya iwe ishara kwa watu watakaokuwa hawamchi Mungu baada ya haya;


Bwana ajua kuwaokoa wamchao na majaribu, na kuwaweka wasio haki katika hali ya adhabu hatta siku ya hukumu;


Lakini mbingu za sasa na inchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hatta siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wana Adamn wasiomcha Mungu.


Hivi pendo limekamilishwa kwetu, tuwe na ujasiri katika siku ya hukumu; kwa kuwa, kama yeye alivyo, ndivyo tulivyo na sisi ulimwenguni humu.


Na malaika wasioilinda enzi yao, wakayaacha makao yao, amewaweka kwa hukumu ile kuu katika vifungo vya milele chini ya giza.


Kama vile bodoma na Gomora, na miji iliyozunguka, waliofuata uasharati kwa jinsi moja na hawa, wakaenda kufuata mambo ya mwili yasiyo ya asili, imewekwa kuwa dalili, wamepasiwa hukumu yamoto wa milele.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo