Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 10:1 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

1 AKAWAITA wanafunzi wake thenashara, akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, wawafukuze, na kuponya magonjwa yote na dhaifu zote.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

1 Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuwafukuza pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

1 Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuwafukuza pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

1 Yesu aliwaita wanafunzi wake kumi na wawili, akawapa uwezo wa kuwafukuza pepo wachafu na kuponya magonjwa na maradhi yote.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

1 Ndipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

1 Ndipo Isa akawaita wanafunzi wake kumi na wawili, naye akawapa mamlaka juu ya pepo wachafu, ili waweze kuwatoa na kuponya kila ugonjwa na maradhi ya kila aina.

Tazama sura Nakili




Mathayo 10:1
26 Marejeleo ya Msalaba  

Yesu akamwambia, Amin, nawaambieni, ya kwamba ninyi mlionifuata, katika zamani za kuzaliwa upya, atakapoketi Mwana wa Adamu katika kiti cha utukufu wake, ninyi nanyi mtaketi katika viti thenashara, mkiwahukumu kabila thenashara za Israeli.


Bassi ilipokuwa jioni akaketi chakulani pamoja na wale thenashara.


Hatta alipokuwa akisema, Yuda, mmoja wa wale thenashara akaja, na pamoja nae makutano mengi, wana panga na marungu, wametoka kwa makuhani wakuu na wazee wa watu.


Yesu akazunguka katika Galilaya yote, akifundisha katika sunagogi zao, na kuikhubiri injili ya ufalme, na kuponya ugonjwa na udhaifu wa killi namna katika watu.


Usitutie majaribuni, bali utuokoe na yule mwovu.


Na Yesu alikuwa akizunguka katika miji yote na vijiji, akifundisha katika masunagogi yao, akikhubiri injili ya ufalme, akiponya magonjwa yote na dhaifu zote katika watu.


Bassi mwombeni Bwana wa mavuno, apeleke watenda kazi katika mavuno yake.


Tazameni, nawapeni mamlaka va kuwakanyaga nyoka na nge, na nguvu zote za yule adui, wala hapana kitu kitakachowadhuru ninyi kamwe.


Kwa maana mimi nitawapeni kinywa na hekima, ambayo watesi wenu hawataweza kuikana wala kushindana nayo.


Angalieni, bassi, naituma ahadi ya Baba yangu kwenu: lakini kaeni katika mji huu Yerusalemi, hatta mtakapovikwa nguvu zitokazo juu.


Ulipokuwa mchana akawaita wanafunzi wake: akachagua watu thenashara miongoni mwao, ambao aliwaita mitume.


kama vile ulivyompa mamlaka juu ya killa mwenye mwili, illi yote uliyompa awape uzima wa milele.


Yohana akajibu, akasema, Hawezi mtu kupokea neno lo lote isipokuwa amepewa kutoka mbinguni.


Baba ampenda Mwana, amempa vyote mikononi mwake.


Yesu akawajibu, Je! sikuwachagua ninyi thenashara, na mmoja wenu ni Shetani?


Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemi, na katika Yahudi yote, na Samaria, na hatta mwisho wa inchi.


Yule pepo akawajibu, Yesu namjua na Paolo namfahamu, bali ninyi ni nani?


NA ishara kuu ilionekana mbiuguni; mwanamke aliyevikwa jua, na mwezi ulikuwa chini ya miguu yake, na juu ya kichwa chake taji ya nyota thenashara.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo