Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 1:22 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

22 Haya yote yamekuwa, illi litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii akinena,

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

22 Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

22 Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii:

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

22 Basi, haya yote yalitukia ili litimie lile neno Bwana alilosema kwa njia ya nabii:

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

22 Haya yote yalitukia ili litimie lile Mwenyezi Mungu alilonena kupitia nabii, aliposema:

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

22 Haya yote yalitukia ili litimie lile Mwenyezi Mungu alilokuwa amenena kupitia nabii, akisema:

Tazama sura Nakili




Mathayo 1:22
22 Marejeleo ya Msalaba  

illi litimie neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema,


lakini hana mizizi udani yake, hukaa muda mchache; ikitukia shidda au udhia kwa sababu ya lile neno, marra huchukizwa.


illi litimizwe neno lililonenwa mi nabii, akisema, Nitafunua kinywa changu kwa mifano, Nitatoa mambo yaliyostirika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.


akawa huko mpaka alipokufa Herode: illi litimie neno lililonenwa na Bwana kwa ujumbe wa nabii, akisema, Kutoka Misri nalimwita mwaua wangu.


akaenda, akakaa mji uliokwitwa Nazareti: illi litimie neno lililonenwa na manabii, Atakwitwa Mnazorayo.


Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.


illi litimie lile neno lililonenwa na nabii Isaya, akisema, Mwenyewe alitwaa magonjwa yetu, na kuchukua maradhi zetu.


Kwa sababu hizi ni siku ya mapatilizo, yote yaliyoandikwa yapate kutimizwa.


Akawaambia, Haya ndiyo maneno yangu niliyowaambieni, nilipokuwa kwenu, ya kuwa hayana buddi kutimizwa yote niliyoandikiwa katika torati ya Musa, na katika manabii, na katika zaburi.


Ikiwa aliwaita wale miungu waliojiliwa na neno la Mungu (na maandiko hayawezi kutanguka),


Lakini litimie neno lililoandikwa katika sharia yao, Walinichukia burre.


Nilipokuwa pamoja nao ulimwenguni, mimi naliwalinda kwa jina lako: wale ulionipa naliwatunza, wala hapana mmojawapo wao aliyepotea, illa yule mwana wa upotevu maandiko yapate kutimizwa.


illi litimizwe lile neno alilolisema, Hawa ulionipa sikupoteza hatta mmoja wao.


Lakini mambo yale aliyokhubiri Mungu tangu zamani kwa vinywa vya manabii wake wote, ya kama Kristo atateswa, ameyatimiza hivyo.


ambayo Mungu amekwisha kuiahidi kwa vinywa vya manabii wake katika maandiko matakatifu,


Maana Muugu ametia mioyoni mwao kufanya shauri lake, na kufanya shauri moja, na kumpa yule nyama ufalme hatta maneno ya Mungu yatimizwe.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo