Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Mathayo 1:20 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

20 Alipokuwa akifikiri haya, malaika wa Bwana akamtokea katika udoto, akisema, Yusuf, mwana wa Daud, usikhofu kumchukua Mariamu mke wako, maana mimba yake ni kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

20 Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

20 Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

20 Alipokuwa bado anawaza jambo hilo, malaika wa Bwana alimtokea katika ndoto, akamwambia, “Yosefu, mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Maria awe mke wako, maana amekuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

20 Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

20 Lakini mara alipoazimu kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili




Mathayo 1:20
38 Marejeleo ya Msalaba  

Na kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipoposwa na Yusuf, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.


Nao wakiisha kuonywa katika ndoto wasimrudie Herode, wakaenda zao kwao kwa njia nyingine.


Na hawo walipokwisha kwenda zao, malaika wu Bwami akamtokea Yusuf katika ndoto, akiuena, Ondoka, umchukue mtoto na mama yake, ukimbilie Misri, ukakae huko mpaka nikuambiapo; kwa maana Herode anataka kumtafuta mtoto amwangamize.


Hatta alipofariki Herode, malaika wa Bwana akamtokea Yusuf katika ndoto huko Misri, akinena,


Lakini aliposikia ya kwamba Arkelao anamiliki Yahudi mahali pa Herode baba yake, akaogopa kwenda huko; akaonywa katika ndoto, akaenda zake hatta pande za Galilaya,


Na alipokuwa ameketi juu ya kiti cha hukumu, mkewe alimpelekea mjumbe, kumwambia, Usiwe na neno na yule mwenye haki: kwa sababu nimeteswa mengi leo katika udoto kwa ajili yake.


Malaika akajibu, akawaambia wale wanawake, Msiogope ninyi; kwa maana najua ya kuwa mnanitafuta Yesu aliyesulibiwa.


Malaika akamjibu, akamwambia, Mimi ni Gabrieli nisimamae mbele ya Mungu: nami nalitumwa niseme nawe, na kukupasha khabari hizi njema.


Na Yusuf nae akaondoka Galilaya kutoka mji wa Nazareti, akapanda kwenda Yahudi hatta mji wa Daud, uitwao Bethlehemu, kwa kuwa yeye wa nyumba na jamaa ya Daud,


lakini malaika wa Bwana akafungua milango ya gereza usiku, akawatoa, akasema,


Na tufurahi tukashangilie tukampe ulukufu wake; kwa kuwa arusi ya Mwana Kondoo imekuja, na mkewe amejiweka tayari.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo