Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Mathayo 1:18 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

18 Na kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi. Mariamu mama yake alipoposwa na Yusuf, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

18 Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke, alionekana kuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

18 Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke, alionekana kuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

18 Basi, hivi ndivyo Yesu Kristo alivyozaliwa: Maria, mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla hawajakaa pamoja kama mume na mke, alionekana kuwa mjamzito kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

18 Kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

18 Basi kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho wa Mwenyezi Mungu.

Tazama sura Nakili

Mathayo 1:18
13 Marejeleo ya Msalaba  

KITABU eba ukoo wa Yesu Kristo, mwana wa Daud, mwana wa Ibrahimu.

Alipokuwa katika kusema na makutano, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wakitaka kusema nae.

Wakaingia nyumbani, wakamwona mtoto pamoja na Mariamu mama yake, wakaanguka wakasujudu; nao walipokwisha kufungua hazina zao, wakamtolea tumi, dhahabu, uvumba, na manemane.

Hivi ndivyo alivyonitendea Bwana, siku zile alizoniangalia, kuniondolea aibu yangu mbele ya watu.

illi aandikwe pamoja na Mariamu mkewe ambae ameposwa nae; nae ana mimba.

Kwa biyo ajapo ulimwenguni, anena, Dhambi na toleo hukutaka, lakini mwili uliniwekea tayari:

Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;

Tufuate:

Matangazo

Matangazo