Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 9:40 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

40 Petro akawatoa wote, akapiga magoti, akaomba, akaielekea mayiti, akanena, Tabitha, ondoka. Nae akafumbua macho yake, na alipomwona Petro akajiinua, akaketi.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akaigeukia ile maiti, akasema, “Tabitha, amka.” Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro, akaketi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akaigeukia ile maiti, akasema, “Tabitha, amka.” Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro, akaketi.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Petro aliwatoa nje wote, akapiga magoti, akasali. Kisha akaigeukia ile maiti, akasema, “Tabitha, amka.” Naye akafumbua macho yake, na alipomwona Petro, akaketi.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Petro akawatoa wote nje ya kile chumba, kisha akapiga magoti akaomba, akaugeukia ule mwili akasema, “Tabitha, inuka.” Akafumbua macho yake na alipomwona Petro, akaketi.

Tazama sura Nakili

Matendo 9:40
14 Marejeleo ya Msalaba  

Bali wewe usalipo, ingia chumba chako cha ndani, na ukiisha kufunga mlango wako, usali mbele ya Baba yako aliye kwa siri: na Baba yako aonae kwa siri atakujazi kwa dhahiri.

Hatta makutano walipoondoshwa, akaingia, akamshika mkono wake; yule kijana akasimama.

Nae Yesu akiona ya kuwa makutano yanakusanyika mbio, akamkemea yule pepo mchafu, akamwambia, Ewe pepo bubu ua kiziwi, mimi nakuamuru, mtoke, wala usimwingie tena.

Akiisha akajitenga nao kadiri ya mtupo wa jiwe, akapiga magoti, akaomba, akisema,

Nae akawatoa nje wote, akamshika mkono wake, akapaaza sauti yake, akisema, Kijana, ondoka.

Alipokwisha kunena haya akapiga magoti, akaomba pamoja nao wote.

Hatta tulipotimiza siku zile tukaondoka tukaenda zetu, na watu wote pamoja na wake zao na watoto wao wakatusindikiza hatta nje ya mji, wakapiga magoti pwani wakaomba:

Ikawa baba yake Publio alikuwa hawezi homa na kuhara damu. Paolo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, akamponya

Akapiga magoti, akalia kwa sauti kuu, Bwana, usiwahesabie dhambi hii. Akiisha kusema haya akalala.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo