Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 9:27 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

27 Barnaba akamtwaa, akampeleka kwa mitume, akawaeleza jinsi alivyomwona Bwana njiani, na ya kwamba alisema nae, na jinsi alivyokhubiri pasipo khofu katika Dameski kwa jina lake Yesu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

27 Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila woga kule Damasko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

27 Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila woga kule Damasko.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

27 Hapo, Barnaba alikuja akamchukua Saulo, akampeleka kwa mitume na kuwaeleza jinsi Saulo alivyomwona Bwana njiani na jinsi Bwana alivyoongea naye. Aliwaambia pia jinsi Saulo alivyokuwa amehubiri bila woga kule Damasko.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

27 Lakini Barnaba akamchukua, akampeleka kwa wale mitume. Akawaeleza jinsi Sauli akiwa njiani alivyomwona Bwana Isa, jinsi Bwana alivyosema naye na jinsi alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Isa huko Dameski.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

27 Lakini Barnaba akamchukua, akampeleka kwa wale mitume. Akawaeleza jinsi Sauli akiwa njiani alivyomwona Bwana Isa, jinsi Bwana Isa alivyosema naye, na jinsi alivyohubiri kwa ujasiri kwa jina la Isa huko Dameski.

Tazama sura Nakili




Matendo 9:27
20 Marejeleo ya Msalaba  

Khabari hizo za watu hao zikafika masikioni mwa kanisa lililokuwa katika Yerusalemi: wakaintuma Barnaba, aende hatta Antiokia.


Barnabi tikatoka akaenda Tarso kumtafuta Saul: hatta alipokwisha kumwona akamleta Antiokia.


Na Barnaba na Saul, walipokwisha kuitimiza khuduma yao, wakarejea kutoka Yerusalemi wakamchukua pamoja nao Yohana aitwae Marko.


Bassi hawa walipokuwa wakimkhudumia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niwekeeni Barnaba na Saul kwa kazi ile niliyowaitia.


Bassi baada ya Paolo na Barnaba kushindana na watu hawa na kuhujiana nao sana, ndugu wakaamuru kwamba Paolo na Barnaba na wengine miongoni mwao wapande kwenda Yerusalemi kwa mitume na wazee kwa khabari ya swali hilo.


Bassi walipoona ujasiri wa Petro na Yohana, na kujua ya kuwa ni watu wasio elimu, wasio maarifa, wakastaajabu, wakawatambua ya kwamba walikuwa pamoja na Yesu.


Bassi sasa, Bwana, yaangalie maogofya yao; ukawajalie watumishi wako kunena neno lako kwa uthabiti,


Na Yusuf, aliyeitwa na mitume Barnaba (tafsiri yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kupro,


Anania akaenda zake, akaingia mle nyumbani; akamwekea mikono akisema, Ndugu Saul, Bwana amenipeleka, Yesu, yeye aliyekutokea katika njia uliyoijia, upate kuona tena, ukajazwe Roho Mtakatifu.


Akaneua kwa jina lake Yesu pasipo khofu, akinena na kushindana na Wahelenisti. Nao wakajaribu kumwua.


na mwisho wa watu wote, alionekana na mimi, kama nae aliyezaliwa si kwa wakati wake.


Au je! ni mimi peke yangu na Barnaba tusio na uwezo kutokufanya kazi?


Na Wayahudi wakajigeuza pamoja nae, hatta Barnaba nae akachukuliwa na unafiki wao.


tena walipokwisha kuijua neema niliyopewa, Yakobo, na Kefa, na Yohana, wenye sifa kuwa ni nguzo, walinipa mimi na Barnaba mkono wa kuume wa shirika, illi sisi tuende kwa mataifa, na wao waende kwa watu wa tohara;


Tufuate:

Matangazo


Matangazo