Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 9:2 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

2 akataka ampe khati za kwenda Dameski zilizoandikwa kwa masunagogi, illi akiona watu wa Njia hii, waume kwa wake, awafunge na kuwaleta Yerusalemi.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

2 akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia hiyo, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

2 akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia hiyo, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

2 akaomba apatiwe barua za utambulisho kwa masunagogi ya Kiyahudi kule Damasko, ili akikuta huko wanaume au wanawake wanaofuata Njia hiyo, awakamate na kuwaleta Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

2 naye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mfuasi yeyote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

2 naye akamwomba kuhani mkuu ampe barua za kwenda kwenye masinagogi huko Dameski, ili akimkuta mtu yeyote wa Njia Ile, akiwa mwanaume au mwanamke, aweze kuwafunga na kuwaleta Yerusalemu.

Tazama sura Nakili




Matendo 9:2
23 Marejeleo ya Msalaba  

Jihadharini na wana Adamu; kwa maana watawapelekeni mbele ya baraza, na katika masunagogi yao watawapiga;


Yesu akamwambia, Ndimi niliye njia, na kweli, na uzima; mtu haji kwa Baba bila kwa mimi.


Mtu huyu alikuwa amefundishwa njia ya Bwana; na kwa kuwa roho yake ilikuwa ikiwaka, alianza kunena na kufundisha kwa usahihi khabari za Bwana; nae alijua ubatizo wa Yohana tu.


Hatta wakati huo kukatukia ghasia si haba katika khabari ya Njia ile.


Lakini wengine walikaidi, wakakataa kuamini, wakiitukana ile Njia mbele ya mkutano; bassi, akaondoka akawaacha, akawatenga wanafunzi nao, akahujiana na watu killa siku katika darasa ya mtu mmoja, jina lake Tyranno.


Illa neno hili naliungama kwako ya kwamba kwa Njia ile ambayo waiita uzushi, ndivyo ninavyomwabudu Mungu wa baba zetu, nikiyaamini yote yanayopatana na torati na yaliyoandikwa katika vyuo vya manabii.


Bassi Feliki, alijiokwisha kusikia haya, aliwaakhirisha, kwa sababu alijua khabari za Njia ile kwa usahihi zaidi, akasema, Lusia jemadari, atakapotelemka nitakata maneno yenu.


nikayafanya Yerusalemi: niliwafunga wengi miongoni mwa watakatifu ndani ya magereza, nikiisha kupewa amri na makuhani wakuu; na walipouawa nalitoa idhini yangu.


Bassi katika kazi hiyo nalikuwa nikienda Dameski, nimepewa mamlaka na maagizo na makuhani wakuu.


Lakini baadhi ya watu wa sunagogi lililokwitwa sunagogi la Malibertino, na la Wakurene na la Waiskanderia, na la wale wa Kilikia na Asia, wakaondoka wakajadiliana na Stefano:


Huyo akawafanyia hila baba zetu, na kuwatenda mabaya baba zetu, akiwaamuru watupe watoto wao wachanga, illi wasiishi.


hatta hapa ana mamlaka kwa makuhani wakuu awafunge wote wakuitiao Jina lako.


Na wote waliosikia wakashangaa, wakasema, Siye huyu aliyewateka walioliita Jina hili Yerusalemi? Na hapa amekuja kusudi hili, awafunge na kuwapeleka kwa makuhani wakuu?


Katika Dameski liwali wa Areta mfalme alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, akitaka kunikamata;


wala sikupanda kwenda Yerusalemi kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nalikwenda zangu Arabuni nikarudi teua Dameski.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo