Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 9:16 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

16 Maana nitamwonyesba mambo mengi makuu yatakayompasa kuteswa kwa ajili ya Jina langu.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

16 Mimi mwenyewe nitamwonesha mengi yatakayomlazimu kuteswa kwa ajili ya jina langu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

16 Mimi mwenyewe nitamwonesha mengi yatakayomlazimu kuteswa kwa ajili ya jina langu.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

16 Mimi mwenyewe nitamwonesha mengi yatakayomlazimu kuteswa kwa ajili ya jina langu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

16 Nami nitamwonesha jinsi impasavyo kuteseka kwa ajili ya Jina langu.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

16 Nami nitamwonyesha jinsi impasavyo kuteseka kwa ajili ya Jina langu.”

Tazama sura Nakili




Matendo 9:16
22 Marejeleo ya Msalaba  

Wakati huo watawasaliti ninyi mpate kuteswa, na watawaua; na mtakuwa watu wa kuchukiwa na mataifa vote kwa ajili ya jina langu.


M kheri ninyi watakapowatukana na kuwatesa na kuwanenea killa neno baya kwa uwongo, kwa ajili yangu.


Likumbukeni lile neno nililowaambieni, Mtumwa si mkubwa kuliko Bwana wake. Ikiwa waliniudhi mimi, watawaudhi ninyi nanyi: ikiwa walilishika neno langu, watalishika na lenu.


wakifanya imara roho za wanafunzi na kuwaonya wakae katika imani, na ya kwamba imetupasa kuingia katika ufalme wa Mungu kwa njia ya shidda nyingi.


Alipotufikia akautwaa mshipi wa Paolo akajifunga miguu na mikono, akasema, Roho Mtakatifu asema hivi, Hivyo ndivyo Wayahudi wa Yerusalemi watakavyomfunga mtu mwenye mshipi huu, nao watamtia katika mikono ya watu wa mataifa.


Paolo akajibu, Mnafanyaje, kulia na kunivnnja moyo? kwa maana mimi, licha ya kufungwa tu, ni tayari hatta kuuawa katika Yerusalemi kwa ajili ya jina lake Bwana Yesu.


Tukiisha kuwaona wanafunzi tukakaa huko siku saba, nao wakamwambia Paolo kwa uwezo wa Roho Mtakatifu asipande kwenda Yerusalemi.


hatta hapa ana mamlaka kwa makuhani wakuu awafunge wote wakuitiao Jina lako.


Lakini simama, uingie mjini, utaambiwa yatakayokupasa kutenda.


bali katika killa neno tukijipatia sifa njema, kama wakhudumu wa Mungu, katika saburi nyingi, kalika mateso, katika shidda, katika taabu,


mtu asifadhaishwe na mateso haya: maana ninyi wenyewe mnajua ya kuwa twawekewa haya.


Kwa sababu hiyo nimepata mateso haya, wala sitahayariki: maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki kwamba aweza kukilinda kile nilichakiweka amana kwake hatta siku ile.


tena adha zangu na mateso yaliyonipata katika Antiokia, katika Ikonio, na katika Lustra; killa namna ya adha niliyoistahimili: nae Bwana akaniokoa katika yote.


Mkilaumiwa kwa ajili ya jina la Kristo ni kheri yenu, kwa kuwa Roho ya utukufu na ya Mungu unawakalia; kwa hawo anatukanwa, bali kwenu ninyi anatukuzwa.


Mimi Yohana, ndugu yenu na mwenye kushiriki pamoja nanyi katika mateso na ufalme na uvumilivu wa Yesu Kristo, nalikuwa katika kisiwa kiitwacho Patmo, kwa ajili ya Neno la Mungu, na kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo