Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 9:15 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

15 Lakini Bwana akamwambia, Shika njia; kwa maana huyu ni chombo kiteule kwangu, alichukue Jina langu mbele ya mataifa, na wafalme, na wana wa Israeli.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

15 Lakini Bwana akamwambia, “Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa watu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

15 Lakini Bwana akamwambia, “Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa watu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

15 Lakini Bwana akamwambia, “Nenda tu, kwa maana nimemchagua awe chombo changu, alitangaze jina langu kwa mataifa na wafalme wao na kwa watu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

15 Lakini Bwana Isa akamwambia Anania, “Nenda! Mtu huyu ni chombo nilichochagua kutangaza jina langu kwa watu wa Mataifa na wafalme wao na watu wa Israeli.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

15 Lakini Bwana Isa akamwambia Anania, “Nenda! Mtu huyu ni chombo changu kiteule nilichokichagua, apate kulichukua Jina langu kwa watu wa Mataifa na wafalme wao na mbele ya watu wa Israeli.

Tazama sura Nakili




Matendo 9:15
38 Marejeleo ya Msalaba  

nanyi mtachukuliwa mbele ya maliwali na wafalme kwa ajili yangu, illi kuwa ushuhuda kwao na kwa mataifa.


Si ninyi mlionichagua mimi, bali mimi niliyewachagua ninyi, nikawaamuru, mwende zenu mkazae, mazao yenu yakakae: illi lo lote mmwombalo Baba kwa Jina langu, awapeni.


Bassi hawa walipokuwa wakimkhudumia Bwana na kufunga, Roho Mtakatifu akasema, Niwekeeni Barnaba na Saul kwa kazi ile niliyowaitia.


Na baada ya kuwasalimu, akawaeleza mambo yote moja moja Mungu aliyotenda katika mataifa kwa khuduma yake.


Akasema, Mungu wa baba zetu amekuchagua upate kujua mapenzi yake, na kumwona Mwenye haki, na kuisikia sauti itokayo katika kinywa chake.


Nae akaniambia, Enenda zako; kwa kuwa mimi nitakutuma mbali kwa watu wa mataifa.


Agrippa akamwambia Festo, Mimi nami nalikuwa nikitaka kumsikia mtu huyu. Akasema, Utamsikia kesho.


AGRIPPA akamwambia Paolo, Una rukhusa kusema mimeno yako. Ndipo Paolo akanyosha mkono wake, akajitetea.


Agrippa akamwambia Festo, Mtu huyo angeweza kufunguliwa kama asingalitaka rufaani kwa Kaisari.


Usiogope, Paolo, huna buddi kusimama mbele ya Kaisari: tena, tazama, Mungu amekupa watu wote wanaosafiri pamoja nawe.


Ikawa baada ya siku tatu akawaita wakuu wa Wayahudi wakutane; hatta walipokuja akawaambia, Wanaume ndugu, ningawa sikufanya neno kinyume cha watu wetu wala neno lililopingamana na desturi za baba zetu, nalitiwa katika mikono ya Warumi, nimefungwa, tokea Yerusalemi.


Bassi ijulikane kwenu ya kwamba wokofu huu wa Mungu umepelekwa kwa mataifa, nao watasikia.


PAOLO, mtumwa wa Yesu Kristo, aliyeitwa kuwa mtume, na kuwekwa aikhubiri Injili ya Mungu,


ambae katika yeye tulipokea neema na utume illi mataifa yote wapate kujitiisha kwa imani, kwa ajili ya jina lake;


Lakini nasema na ninyi, watu wa mataifa. Kwa kadiri nilivyo mtume wa watu wa mataifa, naifukuza khuduma iliyo yangu.


Lakini kwa neema ya Mungu nimekuwa nilivyo; na neema yake iliyo kwangu ilikuwa si burre, bali nalizidi sana kushika kazi kupita wao wote; wala si mimi, bali neema ya Mungu pamoja nami.


Maana, ijapokuwa naikhubiri Injili, sina la kujisifia; maana nimepewa sharti; tena ole wangu nisipoikhubiri.


PAOLO, mtume (si mtume wa wana Adamu, wala hakutumwa na mwana Adamu, bali na Yesu Kristo, na Mungu Baba aliyemfufua),


KWA sababu biyo mimi Paolo, mfungwa wake Kristo Yesu kwa ajili yenu ninyi Mataifa,—


kwa ajili ya huo naliwekwa niwe mkhubiri na mtume (nasema kweli katika Kristo, sisemi uwongo), mwalimu wa mataifa katika imani na kweli.


aliyonifauya mkhubiri na mtume na mwalimu wa mataifa.


Hakuna mfanya vita ajitiae katika shughuli za dunia; illi ampendeze yeye aliyemwandika awe askari.


Hawa watafanya vita na Mwana kondoo, na Mwana kondoo atawashinda, kwa maana ni Bwana wa Mabwana, na Mfalme wa Wafalme; nao walioitwa wateule, waaminifu, watashinda pamoja nae.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo