Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 9:10 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

10 Bassi palikuwapo mwanafunzi Dameski, jina lake Anania. Bwana akamwambia katika njozi, Anania. Akasema, Mimi hapa, Bwana.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

10 Basi, huko Damasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwaye Anania. Bwana akamwambia katika maono, “Anania!” Anania akaitika, “Niko hapa, Bwana.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

10 Basi, huko Damasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwaye Anania. Bwana akamwambia katika maono, “Anania!” Anania akaitika, “Niko hapa, Bwana.”

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

10 Basi, huko Damasko kulikuwa na mfuasi mmoja aitwaye Anania. Bwana akamwambia katika maono, “Anania!” Anania akaitika, “Niko hapa, Bwana.”

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

10 Huko Dameski kulikuwa na mwanafunzi mmoja jina lake Anania. Bwana Isa alimwita katika maono, “Anania!” Akajibu, “Mimi hapa Bwana.”

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

10 Huko Dameski alikuwepo mwanafunzi mmoja jina lake Anania. Bwana Isa alimwita katika maono, “Anania!” Akajibu, “Mimi hapa, Bwana.”

Tazama sura Nakili




Matendo 9:10
23 Marejeleo ya Msalaba  

Akaona katika njozi wazi wazi, panapo saa tissa ya mchana, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, Kornelio!


Nalikuwa katika mji wa Yoppa, nikiomba, roho yangu ikazimia, nikaona maono; chombo kama nguo kubwa kikishuka, kinashushwa kutoka mbinguni kwa pembe zake nne, kikanifikilia.


Akatoka, akamfuata; wala hakujua ya kuwa ni khabari ya kweli iliyofanyika na malaika; bali alidhani anaona njozi.


Bassi alipokwisha kuona yale maono, marra tukataka kutoka kwenda Makedonia, kwa kuwa tuliona hakika ya kwamba Bwana ametuita tuwakhubiri Injili.


Paolo akatokewa na maono usiku; alimwona mtu wa Makedonia amesimama, akimsihi akimwambia, Vuka uje Makedonia utusaidie.


Bwana akamwambia Paolo kwa njozi nsiku, Usiogope, bali nena, wala usinyamaze,


Itakuwa siku za mwisho, asema Mungu, Nitawamwagia watu wote Roho yangu, Na wana wenu na binti zenu watatabiri, Na vijana wenu wataona maono: Na wazee wenu wataota ndoto:


Bassi mtu mmoja, Anania, mcha Mungu kwa kuifuata sharia, aliyeshuhudiwa na Wayahudi wote waliokaa huko, akanijia, akasimama karibu nami, akaniambia, Ndugu, Saul, uone.


nae amemwona mtu, jina lake Anania, akiingia, akiweka mikono juu yake, apate kuona tena.


Akawa siku tatu haoni, wala hali, wala hanywi.


Katika Dameski liwali wa Areta mfalme alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, akitaka kunikamata;


wala sikupanda kwenda Yerusalemi kwa hao waliokuwa mitume kabla yangu, bali nalikwenda zangu Arabuni nikarudi teua Dameski.


Tufuate:

Matangazo


Matangazo