Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -

Matendo 8:9 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

9 Na mtu mmoja, jina lake Simon, alikuwa amefanya uchawi katika mji ule tokeapo, akiwashangaza watu wa taifa la Wasamaria, akisema ya kuwa yeye ni mtu mkubwa.

Tazama sura Nakili

Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

9 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

9 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

9 Basi, kulikuwa na mtu mmoja aitwaye Simoni ambaye alikuwa amekwisha fanya uchawi wake katika mji huo kwa muda na kuwashangaza watu wa Samaria, akijiona kuwa yeye ni mtu maarufu.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

9 Basi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kwamba yeye ni mtu mkuu,

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

9 Basi mtu mmoja jina lake Simoni alikuwa amefanya uchawi kwa muda mrefu katika mji huo akiwashangaza watu wote wa Samaria. Alijitapa kwamba yeye ni mtu mkuu,

Tazama sura Nakili

Matendo 8:9
20 Marejeleo ya Msalaba  

Yeye anenae kwa nafsi yake tu, hutafuta utukufu wake mwenyewe; bali yeye anaetafuta utukufu wake aliyempeleka, huyu ni wa kweli wala ndani yake hamna udhalimu.

Walipokwisha kupita katikati ya kisiwa chote cha Kupro, wakaona mtu mmoja, mchawi, nabii wa nwongo, Myahudi jina lake Bar-Yesu:

Lakini Eluma, yule mchawi (maana ndio tafsiri ya jina lake), akashindana nao, akitaka kumtia yule liwali moyo wa kuiacha Imani.

Kwa sababu kabla ya siku hizi aliondoka Theuda, akidai ya kuwa yeye ni mtu, mkuu watu wapata aroba mia wakashikamana nae, na wote waliomsadiki wakatawanyika wakawa si kitu.

Wakamwangalia, kwa maana muda mwingi amewashangaza kwa uchawi wake.

yule mpingamizi, ajiinuae nafsi yake juu ya killa kiitwacho Mungu ama kuabudiwa; hatta yeye mwenyewe huketi katika hekalu la Mungu, kama Mungu, akijionyesha nafsi yake kana kwamba ndive Mungu.

Maana watu walakuwa wenye kujipenda nafsi zao, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kufuru, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi, wasiowapenda wa kwao,

wenye mfano wa utawa, lakini wakikana nguvu zake; ujiepushe na hao.

wakinena maneno ya kiburi makuu mno, kwa tamaaza mwili na kwa uasharati huwakhadaa watu waliokwisha kuwakimbia wao waishio katika udanganyifu:

Bali nje wako mbwa na wachawi na wazinzi na wauaji nao waabuduo sanamu, na killa mtu apendae uwongo na kuufanya.

Tufuate:

Matangazo

Matangazo