Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 8:40 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

40 Filipo akaonekana katika Azoto, na alipokuwa akipita akakhubiri Injili katika miji yote, hatta akafika Kaisaria.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

40 Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Injili mpaka alipofika Kaisarea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

40 Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Injili mpaka alipofika Kaisarea.

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema: Toleo la Kujifunza

40 Filipo akajikuta yuko Azoto, akapita katika miji yote akihubiri Injili mpaka alipofika Kaisarea.

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

40 Filipo akajikuta Azoto; akasafiri akihubiri Injili katika miji yote hadi akafika Kaisaria.

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

40 Filipo akajikuta yuko Azoto, akasafiri akihubiri Injili katika miji yote mpaka alipofika Kaisaria.

Tazama sura Nakili




Matendo 8:40
21 Marejeleo ya Msalaba  

PALIKUWA na mtu Kaisaria, jina lake Kornelio, akida wa kikosi kilichoitwa Kiitaliano,


Hatta siku ya pili yake wakaingia Kaisaria. Na Kornelio alikuwa akiwangojea, amekusanya jamaa zake na rafiki zake.


Kumbe! marra hiyo watu watatu wakasimama mbele ya nyumba niliyokuwamo, waliotumwa kwangu kutoka Kaisaria.


Na Herode alipomtafuta, asimwone, akawauliza walinzi, akaamuru wanawe. Nae akatelemka kutoka Yahudi kwenda Kaisaria, akakaa huko.


Akatweka, akatoka Efeso, na alipokwisha kushuka Kaisaria, akapanda juu, akawasalimu Kanisa, akatelemkia Antiokia.


Baadhi ya wanafunzi wa Kaisaria wakafuatana na sisi, wakachukua na Mnason, mtu wa Kupro, mwanafunzi wa zamani ambae ndiye tutakaekaa kwake.


Assubuhi yake sisi tulifuatana na Paolo tukatoka, tukafika Kaisaria, tukaingia nyumbani mwa Filipo, Mwinjilisti, aliyekuwa mmoja wa wale saba, tukakaa kwake.


Akaita maakida wawili, akasema, Wekeni tayari askari miateen kwenda Kaisaria, na askari wapanda farasi sabaini, na wenye mikuki miateen, panapo saa tatu ya usiku.


Na wale walipofika Kaisaria, wakampa liwali ile barua, wakamweka Paolo mbele yake. Nae alipokwislia kuisoma, akawauliza, Mtu huyu ni wa wilaya gani?


HATTA Festo alipokwisha kuingia katika wilaya yake, baada ya siku tatu akapanda kwenda Yerusalemi kutoka Kaisaria.


Siku kadha wa kadha zilipokwisha kupita, Agrippa mfalme na Bereniki wakafika Kaisaria, wakimwamkia Festo.


Festo akajibu ya kama Paolo atalindwa Kaisaria; nae mwenyewe yu tayari kwenda huko karibu.


Alipokwisha kukawia kwao siku kumi na zaidi, akatelemkia Kaisaria: hatta siku ya pili akaketi katika kiti cha hukumu akaamuru Paolo aletwe.


Nao walipokwisha kushuhudia na kulikhubiri neno la Bwana wakarudi Yerusalemi wakaikhubiri Injili katika vijiji vingi vya Wasamaria.


Lakini ndugu walipopata khabari wakamchukua hatta Kaisaria wakampeleka Tarso.


katika nguvu za Roho Mtakatifu; hatta ikawa tangu Yerusalemi, na kando kando yake, hatta Illuriko nimekwisha kuikhubiri Injili ya Kristo kwa utimilifu,


Tufuate:

Matangazo


Matangazo