Biblia Todo Logo
Biblia ya mtandaoni

- Matangazo -




Matendo 8:37 - New Testament in Swahili (Zanzibar) Revised Edition 1921

37 Filipo akasema, Ukiamini kwa moyo wako wote, ni halali. Akajibu, akanena, Namwamini Mwana wa Mungu kuwa ndiye Yesu Kristo.

Tazama sura Nakili


Matoleo zaidi

Biblia Habari Njema

37 Filipo akasema, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Naye akajibu, “Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”]

Tazama sura Nakili

Biblia Habari Njema - BHND

37 Filipo akasema, “Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Naye akajibu, “Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu.”]

Tazama sura Nakili

Neno: Bibilia Takatifu

37 Filipo akamwambia, “Ukiamini kwa moyo wako wote, unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Isa Al-Masihi ni Mwana wa Mungu.”]

Tazama sura Nakili

Neno: Maandiko Matakatifu

37 Filipo akamwambia, “Kama ukiamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa.” Akajibu, “Naamini kuwa Isa Al-Masihi ni Mwana wa Mungu.”]

Tazama sura Nakili




Matendo 8:37
20 Marejeleo ya Msalaba  

Simon Petro akajibu, akasema, Wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu aliye hayi.


Bassi, enendeni, kawafanyeni mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu;


Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa.


Akamwambia, Naam, Bwana; mimi nimeamini ya kwamba wewe ndiwe Kristo, Mwana wa Mungu, yule ajae ulimwenguni.


lakini hizi zimeandikwa mpate kuamini kwamba Yesu ni Kristo, Mwana wa Mungu; na kwa kuamini mwe na uzima kwa jina lake.


Bassi Simon Petro akamjibu, Bwana! twende kwa nani? Wewe una maneno ya uzima wa milele.


Yesu akasikia kwamba wamemtoa nje; akamwona, akasema, Wewe wamwamini Mwana wa Mungu?


Petro akawaambia, Tubuni mkabatizwe killa mmoja kwa jina lake Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi, nanyi mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.


Lakini walimpomwamini Filipo, akizikhubiri khabari njema za ufalme wa Mungu, na jina lake Yesu Kristo, wakabatizwa, wanaume na wanawake.


Huna fungu wala huna sehemu katika jambo hili, kwa kuwa moyo wako si mnyofu mbele ya Mungu.


Wakawa wakiendelea njiani, wakafika mahali penye maji: yule tawashi akasema, Yanizuia nini nisibatizwe?


Akaamuru lile gari lisimame: wakatelemka wote wawili majini. Filipo na yule tawashi: akambatiza.


Marra akamkhubiri Yesu katika masunagogi, kwamba yeye ni Mwana wa Mungu.


kwa maana kwa moyo watu huamini hatta kupata haki, na kwa kinywa hukiri hatta kupata wokofu.


Kwa hiyo nawaarifu, ya kwamba hapana mtu asemae katika Roho ya Mungu, anenae, Yesu ni anathema; wala hawezi mtu kusema, Yesu ni Bwana, isipokuwa katika Roho Mtakatifu.


Mfano wa mambo haya ni ubatizo, nnaowaokoa na ninyi siku hizi; (sio kuwekea, mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo;


Killa aungamae ya kuwa Yesu ni Mwana wa Mungu, Mungu hukaa ndani yake, nae ndani ya Mungu.


KILLA mtu aaminiye kwamba Yesu ni Kristo amezaliwa na Mungu. Na killa mtu ampendae mwenye kuzaa ampenda na yeye mwenye kuzaliwa nae.


Amwaminiye Mwana wa Mungu anao ushuhuda ndani yake. Asiyemwamini Mungu amemfanya kuwa mwongo, kwa kuwa hakuuamini ushuhuda ambao Mungu amemsbuhudia Mwana wake.


Mwenye kuushinda ulimwengu ni nani, isipokuwa yeye aaminiye ya kwamba Yesu yu Mwana wa Mungu?


Tufuate:

Matangazo


Matangazo